Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TMA yawahakikishia huduma bora na ufanisi wadau wa usafiri wa anga
Habari Mchanganyiko

TMA yawahakikishia huduma bora na ufanisi wadau wa usafiri wa anga

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TMA, Dk. Ladislaus Chang’a
Spread the love

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau wa usafiri wa Anga wa jijini Dodoma katika ukumbi wa TAA, Dodoma tarehe 21 Disemba, 2022,ili kujadili maendeleo na mahitaji ya huduma za Hali ya Hewa kwa usafiri wa Anga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akifungua mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TMA, Dk. Ladislaus Chang’a alisema “Kusudi la mkutano huu ni kutathimini maendeleo na mahitaji ya utoaji wa huduma za Hali ya Hewa kwa ajili ya usafiri wa Anga ili kuongeza tija na ufanisi katika shughuli na kuhakikisha usalama wa usafiri wa Anga,” alisema Dk. Ladislaus Chang’a.

“TMA imeendelea kutambua umuhimu wa mikutano hii kwani imesaidia kuboresha sio tu ubora wa bidhaa zetu bali pia taratibu za utoaji wa huduma katika sekta ya usafiri wa Anga. Nakumbuka, miaka ya nyuma kulikuwa na malalamiko kadhaa juu ya kutafuta njia bora ya kuhakikisha taarifa za Hali ya Hewa kwa marubani zinapatikana kwa njia ya mtandao yaani (online), TMA tulifanyia kazi malalamiko hayo na kuweza kutengeneza mfumo wa Tehama wa usambazaji wa taarifa hizo unaoitwa MAIS na kuanza kufanya kazi rasmi mwaka 2012,” aliongeza Dk. Ladislaus Chang’a.

Dk. Chang’a alisisitiza kuwa TMA inafanya kazi kwa kuzingatia taratibu za Kitaifa na Kimataifa. Akizungumzia kuhusu taratibu za Kimataifa, alieleza kuwa TMA imeendelea kukaguliwa kila mwaka na kuendelea kushikilia cheti cha ubora ISO 9001: 2015 na hivyo kuhakikishia ubora wa huduma zitolewazo kukidhi viwango vya Kimataifa.

Na kuhusu mabadiliko ya tabia ya Nchi, TMA imeendelea kufuatilia kwa karibu changamoto ya mabadiliko ya Hali ya Hewa hususan ongezeko la joto na matukio ya hali mbaya ya Hewa ambayo pia yanaendelea kuathiri huduma katika sekta ya usafiri wa Anga na hivyo kuhitaji uimarishaji wa utoaji na matumizi ya taarifa za Hali ya Hewa.

Awali wakati akifungua Mkutano huo, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya Hali ya Hewa kwa kufanya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kisasa vya hali ya hewa ikiwemo Rada.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!