Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mhagama: Mafuriko Rufiji yametokana na mvua za El-nino
Habari za Siasa

Mhagama: Mafuriko Rufiji yametokana na mvua za El-nino

Spread the love

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amewaeleza wananchi walioathiriwa na mafuriko katika wilaya za Kibiti na Rufiji kwamba maafa haya ya mafuriko yametokana na mvua kubwa za El Nino zinazoendelea kunyesha katika sehemu kubwa ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akiwa ameambatana na mawaziri wanne na manaibu mawaziri watano, waliofanya ziara kwenye eneo la maafa ya mafuriko katika wilaya hizo leo Alhamisi, Mhagama ametoa mfano wa Mlimba mkoani Morogoro ambako kumeathiriwa pia na mafuriko na kesho Ijumaa kamati ya Mawaziri itafanya ziara pia.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mutoro Magharibi kwenye kata ya Muhoro katika tarafa ya Muhoro wilayani Rufiji na baadaye kwenye kiji cha Mtunda kwenye kata ya Mtunda katika tarafa

ya Kikale wilayani Kibiti, Waziri Mhagama aliwafikishia wananchi salamu za połe kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan; na kuwahakikishia kwamba serikali ipo pamoja nao na itatoa misaada yote inayohitajika katika kipindi hiki.

Pia aliwataka wananchi kutii maelekezo ya viongozi wao ya kutoka kwenye maeneo hatarishi kabla maafa hayajatokea.

Alisema kuwa Serikali imeshaleta tani 40 za mahindi huku tani 150 za unga wa mahindi, tani 50 za maharage na lita 100 za mafuta ya kupikia zikiwa njiani na kwamba Serikali inaandaa tani zaidi za chakula na madawa.

Alisema tayari wataalam wa afya na ustawi wa jamii wameshaanza kazi katika eneo hilo na wataalam wa sekta zingine wanaendelea kuwasili.

“Kwa ujumla kata 12 kati ya kata 13 za wilaya ya Rufiji na kata tano kati ya 13 za witaya ya Kihiti zimeathirika na walaalam wa serikali wanaendelca na tathmini ili kujua ukubwa wa eneo na athari. Aidha, kambi za kuwahudumia waathirika zinaendelea kufunguliwa kwenye wilaya hizo,” alisema.

Mawaziri wengine wa sekta zinazohusika na maafa haya waliokuwa ziarani ni Waziri wa Ulinzi, Dk. Stergomena Tax: Waziri wa Maendelco ya Jamii, Jinsia, Wanawake na akundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendcleo ya Makazi, Jerry Silaa.

Wengine ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso. Manaibu Mawaziri walikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati, Joyee Kapinga: Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kiandula: Naibu Waziri wa Uienzi, Godfrey Kasekenya: na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Siro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!