Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao
Habari Mchanganyiko

Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao

Spread the love

 

WAZAZI na walezi wameagizwa kuwalea watoto wao katika maadili mema yenye kuwa na hofu ya Kimungu pamoja na wanafamilia hao kuishi kwa upendo na amani ili kuondokana na migogoro ya kifamilia. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Maagizo hayo yametolewa jana tarehe 10 April 2024 na Sheikh Mohamed Khamis wa Msikiti wa Al Madarasatu Nuraniyyah ulioopo mtaa wa Chamelo Jijini Dodoma wakati wa mawaidha ya siku ya Eid El Fitir yaliyofanyika katika msikiti huo.

Kiongozi huyo wa Kiroho amesema kuwa mmomonyoko wa maadili unatokana na wazazi au walezi kutokuwalea watoto wao katika misingi ya Kuncha Mungu na wakati huo huo familia kuendekeza migogoro isiyoisha.

Amesema kuwa familia nyingi haziwi karibu na watoto hivyo hawawezi kuelewa zaidi changamoto ambazo watoto wanakutananazo na wakati mwingine kutokujua makundi ya watoto wao yana tabia za aina gani.

Amesema zipo familia ambazo hazina hata muda wa kukutana na watoto wao kukaa nao na kuongea nao na kuwapa misingi iwapasayo kuifata jambo ambalo kiongozi huyo amesema ni kusababisha mmomonyoko wa maadili.

“Ni wajibu wa wazazi au walezi kukaa na watoto wenu,kuwa karibu nao na kuzungumza nao mara kwa mara na kuwajengea misingi mizuri yenye hofu ya Kimungu na mkifanya hivyo ni wazi tutakuwa na taifa la vijana wema na viongozi waadilifu.

“Pia mkipata muda wa kukaa na hao watoto mtapata muda mzuri wa kujua changamoto zao na matatizo wanayokutana nayo na hapo mtaweza kuzungumza na vijana wenu na wakati mwingine hata kuwaonesha ndugu,jamaa ambao ni wahusika katika familia husika kwa malezi bora zaidi”Ameeleza Sheikh Khamisi.

Akiwaongerea waumini wa dini ya Kiislamu amewataka kutunza utakatifu wao waliounesha wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhani na wasiwe na matendo maovu maada ya kumaliza mfungo wa Ramadhani.

Amesema siku ya Eid iwe siku ya kukaa na familia na kutafakari matendo makuu ambayo Mungu amewatendea katika kipindi chose cha Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuendeleza mema hayo.

“Siku ya Eid isiwe siku ya kuvaa nguo mpya na kufanya anasa,bali iwe siku ya kutafakari ukuu wa Mungu na kuwatendea mema wale wote ambao wana uhitaji na kuendeleza kueneza dini ya Uislamu”amesisitiza Sheikh Khamisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!