Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Meena: Hukumu kwa vyombo vya habari zisiwe za kukomoa
Habari Mchanganyiko

Meena: Hukumu kwa vyombo vya habari zisiwe za kukomoa

Nevile Meena
Spread the love

 

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Nevile Meena, ameishauri Serikali ikamilishe mchakato wa marekebisho ya sheria zinazosimamia tasnia ya habari, ili kuwe na utaraibu mzuri wa kutoa adhabu kwa vyombo vya habari vinavyokiuka maadili. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akihojiwa na televisheni ya mtandao ya Global, leo Jumanne, tarehe 13 Septemba 2022, Meena ameishauri Serikali kupitia marekebisho hayo, iunde chombo huru cha kushughulika na vyombo vya habari vinavyokiuka maadili, ili kuondoa changamoto ya utolewaji hukumu za kukomoa.

“Tunayo mifano ya mageti yaliyowahi kufutwa, tunaomba Serikali iondoe utaratibu wa kufungia vyombo vya habari hasa utaratibu wa mtu mmoja kuamua. Yaani kuwepo mfumo ambao chombo kikikosea tunawajadili,” amesema Meena.

Meena amesema “yeyote anayelalamika apeleke mashtaka kwenye hicho chombo ambacho kinaundwa na wanataaluma ambao wanaelewa taaluma hii. Wakosaji waitwe wajitetee mwishoni chomo kinatoa hukumu na hizo hukumu zisiwe za kukomoa.”

Mdau huyo wa tasnia ya habari amesema, uundwaji wa chombo hicho utasaidia kuweka utaratibu mzuri wa kutoa adhabu zitakazolenga kuongeza uwajibikaji.

“Hicho chombo kitoe hukumu, hiyo hukumu isiswe ya kukomoa bali iwe ya kuongeza uwajibikaji zaidi. Inaweza ikawa faini, kuwapa barua ya onyo ama onyo,” amesema Meena.

Meena amesema utaratibu wa utoaji adhabu kwa vyombo vya habari uliopo sasa, hautoi nafasi ya kutosha kwa wahusika kujitetea pindi wanapokabiliwa na makosa ya ukiukaji maadili.

“Lakini utaratibu wa sasa inakuwaje? TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) kuna kamati ya maudhui, inaandika barua mjitetee, hakuna mtu aliyewahi itwa kamati ya maudhui TCRA akashinda,”

“Anayekuandikia barua siku ya kwanza ndiyo huyo anapokea utetezi wako, anayekusikiliza na siku ya hukumu ndiyo huyo anakuhukumu na kusimamia utekelezaji wa adhabu. Tunasema hapo kuna shida,” amesema Meena.

Aidha, Meena ameshauri watumishi wa vyombo vya habari wanaosababisha makosa ya ukiukaji wa maadili ndiyo wawajibishwe, badala ya chombo husika kuadhibiwa kwani kitendo hicho kinakiuka haki za wengine wasio na makosa.

“Kwa nini kusiwe na utaratibu wa kuadhibu wale watu ambao pengine wameruhusu maudhui yakaenda na wameshindwa kudhibiti? Kwa nini adhabu zisizingatie asili ya chombo chenyewe? Mfano nyie manniuliza maswali kikipanda kichaa nikitukana we utaomba radhi, hiyo radhi utaomba inabidi izingatiwe katika hukumu, kwamba tuliomba radhi kuliko kuhukumiwa bila kujitetea,” amesema Meena.

Mchakato wa marekebisho ya sheria umepamba moto hivi karibuni baada ya TEF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Umoja wa asasi zinazotetea haki ya kupata taarifa Tanzania (CoRI), kuanzisha kampeni maalum ya kuishawishi Serikali kuvifanyia marekebisho baadhi ya vifungu vya sheria, vinavyominya ustawi wa tasnia ya habari nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!