Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Mwamalanga: Mawaziri wanatumia kamba vibaya
Habari za Siasa

Askofu Mwamalanga: Mawaziri wanatumia kamba vibaya

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Askofu William Mwamalanga
Spread the love

KAMATI ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu Dini nchini imemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuziondoa kamba alizowapatia mawaziri kwani baadhi yao wamezigeuza kuwa mirija ya kuliibia taifa.

Imesema mawaziri hao wametumia mamlaka yao kwa kuwajazia tozo kwenye huduma za mafuta, simu na benki hivyo kusababisha maisha kuwa magumu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Askofu William Mwamalanga wakati akifungua mkutano wa viongozi wa dini uliofanyika mkoani Morogoro leo Septemba 13,2022.

Askofu Mwamalanga ameonya kuwa tozo zinazolalamikiwa na wananchi walipashwa wakatwe mawaziri na wabunge ambao hawalipi baadhi ya kodi na mishahara yao ni mikubwa.

Alisema kauli ya Rais Samia kuwataka wateule wale wale kwa urefu wa kamba zao inaweza kuwa imepokelewa vibaya hivyo wanamuomba aibatilishe Kwani wapiga kura wanaumia.

“Mawaziri na wabunge wana mishahara mikubwa nadhani wao ndio wanapaswa kutozwa tozo mbalimbali na sio sisi walalahoi, tunamuomba Rais Samia aangalie hawa wasaidizi wake wametumia urefu wa kamba vibaya,”alisema.

Amesema tozo zimegeuka shubiri kwa mananchi kwani zimezidi useful hadi kwenye mifuko ya wanyonge, wajane, wazee, yatima, vilemavu na wagonjwa jambo ambalo limetengeneza dhambi kubwa mbele za Mungu kwani kula msaada wa yatima ni sawa na kula makaa ya moto someni quran na torati.

“Sisi viongozi wa dini tunakushauri Rais Samia ondoa tozo zote alizoweka Waziri Mwigulu Nchemba na badala yake peleka tozo hizo kwenye bandari, madini na maliasili lukuki tulizo nazo,” amesema Askofu Mwamalanga.

Amesema iwapo Rais Samia hatofanya hivyo atakuwa ameligawa taifa kwa wasio nacho na walionacho jambo ambalo limetolewa mfano na Profesa Sospiter Muhongo na Profesa Mussa Assad.

Askofu Mwamalanga amesema maprofesa hao wamekuwa wakionyesha njia bora za kufikia uchumi wa haraka lakini kinachowashangaza ni jinsi ambavyo ushauri wao hautumika wakati majirani wanautumia ndiyo maana leo Zambia inakwenda kwa kasi bila tozo kwa wananchi wake.

“Leo hii kila kona ya nchi yetu vilio vya wizi wa matozo anasimama waziri anasema wananchi walimpa kibali cha kuanzisha matozo tukiendelea kuwalea mawaziri waongo wadanganyifu ambao kutwa wanafanya kampeni za urais taifa litaingia kwenye dhoruba hatari vijijini wananchi wanaandikisha majina lakini mbolea hazitoshelezi,” ameonya Askofu Mwamalanga.

Mwamalanga amewakumbusha watanzania maneno ya Mwalimu Julius Nyerere aliye onya tamaa za wanasisa kukimbilia Ikulu ambapo na yeye amewaonya watanzania kujiepushe na watu wanaoingia siasa kwa lengo la kukimbilia Ikulu.

Amesema uchunguzi wao umebani kuwa baadhi ya mawaziri wana uwezo mdogo wa kuleta mabadiliko chanya ya kulikwamua taifa kutoka kwenye dimbwi la umasikini kwani kitendo cha kuziifumbia macho kodi na tozo kutoka kwenye bandari, madini na maliasili lukuki za nchini kinatoa picha mbaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!