Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watu 116 mbaroni tuhuma za uvunjaji nyumba Dar
Habari Mchanganyiko

Watu 116 mbaroni tuhuma za uvunjaji nyumba Dar

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP William Mkonda
Spread the love

 

WATU 116 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuvunja nyumba na uporaji wa mali za raia kwa kutumia sialaha za jadi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ialiyotoa leo Jumanne, Kaimu Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, ACP William Mkonda, amesema watuhumiwa hao walikamatwa kati ya tarehe 10 hadi 12 Septemba, 2022, kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche, dhidi ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Katika kipindi cha siku tatu limewakamata wahalifu 116 wa makosa ya uvunjaji nyumba na uporaji wa makundi kwa kutumia na silaha za jadi,”imesema taarifa ya Kamanda Mkonda.

Taarifa ya Kamanda Mkonda imesema kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na vielelezo mbalimbali, ikiwemo mapanga, visu na vifa vya kuvunjia nyumba na televisheni.

“Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano ya kina na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuhuma zao. Oparesheni hii kali inaendelea, usiku na mchana, dhidi ya mtu au kikundi cha kihalifu, uvunjaji nyumba na uhalifu mwingine,” imesema taarifa ya Kamanda Mkonda.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mkonda amesema tarehe 12 Septemba 2022, Polisi walikamata silaha aina ya Rifle, ikiwa na risasi mbili inayodaiwa kutumiwa na watuhumiwa wa ujambazi kumjeruhi mfanyabiashara Denis Komba, na kupomra fedha kiasi cha Sh. 2,000,000.

“Polisi kwa kutumia wataalamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi waliwafuatilia majambazi hao na kugundua walikuwa wakielekea eneo la Mwasonga Kigamboni, Dar es salaam. Askari Polisi waliweka mtego katika eneo hilo na majambazi hao walipokaribia katika eneo aligundua kufuatiliwa hivyo kutupa begi lililokuwa na silaha na kutokomea porini,” imesema taarifa ya kamanda Mkonda na kuongeza:

“Na katika upekuzi katika begi hilo ilipatikana silaha hiyo ikiwa na risasi mbili. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawasaka majambazi hawa popote watakapo kimbilia kwani jitihanda za kupambana na uhalifu hazina mipaka.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!