Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Mwanga apiga kambi jimboni, aahidi miradi kukamilika
Habari za Siasa

Mbunge Mwanga apiga kambi jimboni, aahidi miradi kukamilika

Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo (CCM) amefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo na kusikia kero za wananchi katika vijiji vinne vya kata ya Toloha na Kwakoa wilayani humo mkoani Kilimanjaro. Anaripoti Safina Sawart, Kilimanjaro…(endelea).

Katika ziara hiyo Tadayo ameambatana na Wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ,ambapo walikagua miradi ya elimu pamoja na kufanya mikutano ya hadara na kusikiliza kero za wananchi.

Akizungumza wananchi baada kukagua miradi Tadayo amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu imepeleka fedha nyingi katika jimbo la Mwanga kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo hospitali ya wilaya, jengo la halmashauri , ujenzi wa shule mpya za kata Kivisini na Toloha, ujenzi chuo cha kisasa cha ufundi.


Amesema miradi mingine ni pamoja miradi ya barabara, maji na kilimo cha mwagiliaji na kwamba lengo la serikali ni kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Hata hivyo, Tadayo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao ili iweze kutekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa kulingana na fedha zilizotolewa.

Amasema kuwa serikali ipo makini katika kutekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 na kwamba imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa.

Amesema katika kuhakikisha wananchi wanakuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi – CCM Serikali imeweka kipaumbele kusikiliza kero za wananchi na ikiwa ni pamoja na kuchukua maoni.


Amesema jimbo la Mwanga ni miongoni mwa majimbo ambayo yamenufaika na miradi mikubwa ya kimkakati na kwamba bado fedha zinaendelea kuletwa .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano hiyo baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wameipongeza serikali kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita huku wakiomba serikali kukamilisha mradi mkubwa wa maji Same -Mwanga -Korogwe ili kutatua kero za maji.

Latifa Ngumuo amesema mradi huo ukikamilika umaliza kero za muda mrefu wa maji katika vijiji hivyo.

Sambamba na kero ya maji pia wamelalamikia kero ya uvamizi wa tembo na kusababisha uharibifu wa mazao ya chakula hali iyopelekea upungufu wa chakula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!