UFAULU wa mtihani wa kidato cha sita kwa 2023, umeongezeka kwa aislimia 0.2, kutoka 98.97%(2022) Hadi 99.23% mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Hayo yamebainishwa jana Alhamisi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Said Mohamed, akitangaza matokeo ya mtihani huo.
Dk. Mohamed amesema ufaulu huo ni kwa watahaniwa waliosajiliwa 106,883 (wavulana 59,543, wasichana 47,340), ambapo 104,549 wamefaulu.
Dk. Mohamed alisema wavulana waliofauli ni 57,843 wakati wasichana ni 46,707.
Leave a comment