MEYA wa Manispaa ya Moshi, Zuberi Kidumo amekanusha madai ya kupigwa na Diwani wa kata ya Mji Mpya – Moshi, Abuu Shayo (CCM) katika Kikao cha kamati ya mipango miji na ardhi katika manispaa hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).
Taarifa za kupigwa kwa Meya huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Njoro, zimesambaa jana Alhamisi katika mitandao ya kijamii, zikidai kuwa alishushiwa kipigo baada ya ‘kumkwida’ Diwani Shayo aliyehoji ubadhirifu katika halmashauri hiyo.
Aidha, akizungumza leo tarehe 14 Julai 2023 na waandishi wa habari wilayani Hai, Meya Kidumo ameeleza kushangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona kwenye mitandao ya kijamii.
Amefafanua kuwa ni kweli kulikuwa na kikao cha Kamati ya Mipango miji na Ardhi katika manispaa hiyo kilichofanyika jana saa nne hadi saa saba.
“Baada kikao kuisha watu walipata chakula na mimi nilienda kwenye kikao cha halmashauri kuu ya kata Njoro ambayo nini ni diwani wake.
“Nilipotoka Njoro nikaelekea uwanja ambako kulikuwa na mechi lakini cha ajabu ndipo nikaona hizo taarifa,” amesema.
Leave a comment