Tuesday , 3 October 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mbunge azua taharuki akifyatua risasi bungeni
Kimataifa

Mbunge azua taharuki akifyatua risasi bungeni

Spread the love

MBUNGE wa M’baiki Mashariki nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Alfred Yekatom amekamatwa ndani ya bunge baada ya kufyatua risasi hewani, wakati wabunge wakijiandaa kumchagua spika mpya. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Tukio hilo limetokea jana Jumatatu, ambapo Yekatom alifyatua risasi wakati akijaribu kukimbia, lakini hakufanikiwa na kuishia mikononi mwa polisi.

Yekatom ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa kijeshi na kikundi cha wapiganaji cha Anti-Balaka Militia kilichokuwa kinatetea jumuiya za wakristo dhidi ya kikundi cha wapiganaji wenye itikadi ya kiislamu-Seleka , alizua taharuki na kusababisha baadhi ya wabunge kukimbilia nje.

Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kati lilikuwa linamchagua spika mpya siku tatu baada ya kuondolewa Spika Karim Meckassoua, anayewakilisha mji wenye waislamu wengi wa Bangui.

Baada ya uwepo wa mapambano makali baina ya vikundi vya waislamu na wakristo nchini humo, Meckassoua alichaguliwa mwaka 2016 kuwa spika, kitendo kilicholeta matumaini kuhusu upatanisho wa taifa hilo.

Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa, kisa cha kuondolewa Meckassoua ni kutokuwa na ushirikiano mzuri na Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera ambaye ni mkristo.

Baada ya kuondolewa kwenye wadhifa huo, Meckassoua siku ya Jumapili alitangaza kwenda mahakamani kupinga hatua hiyo, akidai kuwa ilisukumwa na tofauti za kidini kwa kuwa watu 38 kati ya 41 waliopiga kura ya kumuondoa, walikuwa ni wakristo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Urusi yafungua milango kwa nchi za Afrika

Spread the loveSERIKALI ya Urusi imefungua milango ya ushirikiano wa kiuchumi, kijamii...

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Putin aita vikundi vya kujitolea vita ya Ukraine

Spread the loveRAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amefungua milango ya ushirikiano kwa...

Kimataifa

Mlipuko wa bomu waua 50 katika sherehe za Maulidi ya Mtume

Spread the loveWATU takribani 50 wamefariki dunia huku wengine 50 wakijeruhiwa katika...

error: Content is protected !!