March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tibaijuka azungumzia sekeseke la utekaji

Anna Tibaijuka, Mbunge wa Muleba Kusini

Spread the love

MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka amewataka watanzania kuwa makini kuhusu usalama wao kutokana na uwepo wa makundi ya wahuni na watekaji wanaojaribu kutaka kuvuruga amani iliyopo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tibaijuka ameyasema hayo wakati akizungumza na vijana 177 waliohitimu mafunzo ya mgambo (jeshi la akiba) katika Kata ya Kalambi jimboni Muleba Kusini.

“Wananchi tukae mkao wa kudadisi mambo, ukiona mtu haeleweki humjui toa taarifa, ukiona kifurushi kimewekwa mahali usiwe mwepesi kuangalia nini usikute bomu limetegeshwa. Watu wabaya sana, wanataka kuharibu amani iliyopo kuivuruga,” amesema Prof. Tibaijuka.

Kuhusu vijana hao wa jeshi la akiba, Prof. Tibaijuka amesema kuna mpango wa kufunguliwa kampuni ya ulinzi ili vijana hao wapate ajira sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama jimboni mwake hasa bomba la mafuta la Tanzania na Uganda linalotokea Tanga hadi Hoima nchini Uganda.

Vile vile ametoa ametoa fedha kwa ajili ya kununua sare za vijana hao walio maliza mafunzo jimboni kwake.

“Nilikua nawakumbusha miadi yetu kwamba tunakwenda kufungua kampuni ya ulinzi kusudi iwasaidie kupata ajira. Mimi kama mbunge wao lazima niwasaidie lakini huwezi pata ajira kabla ya kuweka miundombinu ya ajira.

Sasa ulinzi ni lazima, lazima uwe na vyombo vya ulinzi, ndio maana nakazana waunde kampuni, ulinzi umekuwa biashara ni fani inayopanuka sababu wahuni wamekuwa wengi, watekaji na kadhalika. Bomba letu la mafuta Rais John Magufuli amelileta na sisi angalau tuliunge mkono kwa kulilinda “amesema Prof. Tibaijuka.

error: Content is protected !!