Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Operesheni fagia mashoga yaiva
Habari Mchanganyiko

Operesheni fagia mashoga yaiva

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ameshatumiwa majina ya wanaume 100 wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na jumbe 5,763. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kupitia taarifa yake Makonda ameeleza kuwa wanaDar es Salaam wamewachoka na hawapendezwi na tabia ya ushoga hivyo wametoa ushirikiano na ofisi yake.

Zoezi hilo limeibuka mara baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Amber Rutty kuachia video yake ya ngono.

“Nimepokea jumbe zaidi 5,763 na majina ya mashoga zaidi ya 100 hii inaonyesha WanaDSM hawataki laana ya mashonga. Naendelea kupokea majina ya Mashoga,” amesema Makonda.

Makonda amesema msako mkali wa kamata kamata ya mashoga na watu wanaojiuza utaanza wiki ijayo kwani kwa sasa anakiandaa kikosi kazi pamoja na kupokea baadhi ya majina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Vijana (U20) kwa Kagera Sugar FC

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi ya Vijana chini ya miaka 20...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!