Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka udhibiti utitiri wa makanisha yenye mafundisho mabovu
Habari za Siasa

Mbunge ataka udhibiti utitiri wa makanisha yenye mafundisho mabovu

Kilumbe Ng’enda
Spread the love

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda (CCM) ameiomba  Serikali iweke mkazo katika usajili wa makanisa na taasisi za dini za madhehebu mbalimbali, ili kudhibiti yanayodaiwa kufundisha imani zenye madhara kwa jamii. Anaripoti Jemimah Samwel…(endelea).

Akizungumza katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 7 Novemba 2023, Ng’enda alidai kumekuwa na utitiri wa makanisa na taasisi nyingi za dini, kutokana na kukosekana kwa udhibiti katika usajiri wake.

“Serikali inapaswa kuweka usajili katika taasisi na madhehebu ya dini, hiyo itasaidia kupunguza madhara yanayoletwa na taasisi hizo,” amesema Ngenda.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini amesema usajili wa taasisi hizo unafanywa kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya na kwamba kabla hazijasajiliwa hupitiwa ili kubaini kama zimekidhi vigezo.

“Ofisi ya Msajili inaendelea kushughulikia maombi ya usajili wa taasisi na madhehebu ya dini na kutoa usajili kwa wakati kwa taasisi zenye sifa stahiki. Lakini kuhakikisha Serikali haisajili taasisi  ambazo zinaweza kuleta madhara kwa jamii na kuhamasisha vitendo ambavyo ni kinyume na mila na maadili ya kitanzania,” amesema Sagini.

Sagini, amesema jumla ya maombi ya usajili wa taasisi na madhehebu ya dini 1,858 yalipokelewa katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya, ambapo taasisi 419 zilisajiliwa, wakati maombi ya taasisi nne yakikataliwa huku maombi 1,435 yakiwa katika hatua mbalimbali za usajili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!