Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe aanika madudu ya Sabaya, ashukuru Polisi
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe aanika madudu ya Sabaya, ashukuru Polisi

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Chadema, Freeman Mbowe, amedai aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya alikuwa anatumia ofisi yake kuwapa mateso wananchi waliokuwa wanaunga mkono  upinzani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Mbowe ameyasema hayo leo Jumamosi, tarehe 19 Machi 2022, akihutubia wananchi wa Hai, waliompokea akitokea jijini Dar es Salaam, alikokuwa baada ya kutoka mahabusu ya Gereza la Ukonga, tarehe 4 Machi mwaka huu.

Mbowe amedai, Wilaya ya Hai enzi za uongozi wa Sabaya ambaye kwa sasa ni mfungwa katika Gereza la Kisongo, jijini Arusha, ilikuwa kielelezo cha watu kuumizwa.

Mwanasiasa huyo amedai, aliwahi kutoa taarifa za maovu ya Sabaya kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, ambao waliahidi watashughulikia taarifa hizo bila mafanikio.

“Hakuna mahali unakoweza kupatua kielelezo zaidi ya Hai, dhidi ya kunyanyaswa na kuumizwa watu. Mimi nilipiga kelele muda mrefu nikiiambia dunia, nikamwambia Magufuli, waziri mkuu, IGP kwamba Jimbo la Hai mmetupelekea mhuni kuwa kiongozi hao wote wananiambia tutashughulikia nikigeuka wanasema tumepatia,” amedai Mbowe.

“Ofisi ya umma inatumika kutesa wananchi, watu wamekatwa masikio, vidole, wamepigwa shoti za umeme ofisini kwa mkuu wa wilaya. Haya makosa anayoshtakiwa Sabaya ni asilimia moja ya anayoshtakiwa. Hakuna watu wameona kwa vitendo kama wa Hai.”

Katika hatua nyingine, Mbowe amelishukuru Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, kwa kuwaruhusu wananchi wampokee katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), pasipo kuwabughudhi.

“Leo nimepokelewa KIA Polisi wamekuwepo hajapigwa mtu bomu, hajaumizwa mtu yoyote. Polisi tunashukuru sana hii ndiyo Tanzania tunayoitaka. Ulafi wa madaraka kwa wachache walioko kwenye uongozi usitujengee ubaguzi wa aina yoyote,” amesema Mbowe.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!