November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtutura: Wabunge wa CCM wameonewa

Spread the love

KATIBU wa chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa kichama Selou, Abdallah Mtutura amesema kitendo cha CCM kupeleka wabunge wasioweza kuwasema wananchi wao ni kuwaonea wabunge hao. Anaripoti Faki Sosi, Tunduru … (endelea).

“Mtu ukimpa kitu asichoweza kukimudu au kukidhibithi unakuwa umemuonea.”

Kauli hiyo ameitoa leo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu kwenye jimbo la Tunduru Kaskazini kata ya Ligula.

Mtutura amesema kuwa asilimia 70 wabunge wa Chama Cha Mapinduzi hawana uwezo wa kuwasemea wananchi bungeni.

Amesema kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 haukuwa huru wala wa haki na matokeo yake wakapelekwa watu ambao hawakustahili kuwa wabunge ndio sababu ya kushindwa kuwatetea wananchi bungeni.

Amesema kuwa wabunge hawasemi kama wananchi wanaonewa, tembo wanavamia makazi na mashamba ya watu, hawasemi mgogoro wa wakulima na wafugaji unaoweza kusababisha machafuko.

Mtutura ameongeza kuwa wananchi wamezidiwa na shida hakuna wa kuwasemea. Ametoa wito kwa wananchi kukichagua Chama cha ACT ili wapate sauti mbadala.

error: Content is protected !!