BARAZA la Mitihani nchini (NECTA), limetangaza matokeo ya darasa la saba ambapo Mikoa ya Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kushika nafasi 10 za mwanzo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Angalia hapa matokeo yote ya darasa la saba 2019
Akitangaza matokeo hayo leo tarehe 15 Oktoba 2019, Dk. Charles Msonde, katibu mtendaji wa baraza hilo amesema, ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78.
Msonde amesema, asilimia 81 ya watahiniwa wamefauli mtihani huo huku wanafunzi 909, wakifutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu.
Amesema, pamoja na matokeo hayo, tatizo kubwa lipo katika somo la Kiingereza ambalo ufaulu wake umepungua huku akiagiza juhudi zaidi kufanyika.
Kwenye matokeo hayo, mikoa ya Kanda ya Ziwa imeonekana kufanya vizuri zaidi kulinganisha matokeo ya mwaka jana na miaka iliyopita.
Msonde ametaja shule 10 bora kuwa ni Graiyaki (Mara), Twibhoki (Mara), Kemebos (Kagera), Little Treasures (Shinyanga), Musabe (Mwanza), Tulele (Mwanza), Kwema Morden (Shinyanga), Peaceland (Mwanza), Mugini (Mwanza) na Rocken Hill (Shinyanga).
Katika ufaulishaji watoto wengi Msonde amesema, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika nafasi ya kwanza ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.
Kwenye matokeo hayo, Msonde ametaja wanafunzi walioshika nafasi ya 10 za mwanzo kuwa ni Grace Imori Manga (Graiyaki), Mara; Francis Gwani (Paradise) Geita na wa tatu ni Loi Kitundu (Mbezi), Dar es Salaam.
Wengine ni Victor Godfrey, Azizi Yassin na Goldie Hhayuma wote wa Graiyaki, Mara; Daniel Daniel (Little), Shinyanga; Hilary Nassor (Peaceland), Mwanza; Mbelele Mbelele (Kwema Modern), Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki (Mara).
darasa la saba kisukuru
VELONIKA BUGOMBA
Matokeo ya dal mwaka wa nyuma
Matokeo.yadarasa.lasaba2019mkoakagera.rwigembe.p/school
Hai jamani mbona hvo