Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Tumekwama
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: Tumekwama

Spread the love

SERIKALI imekwama kushawishi wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, jambo ambalo linaleta taswira hasi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu. Anaripoti Martin Kamote…(endelea).

Joran Bashange, Mwenyekiti wa Kampeni na Uchaguzi Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Oktoba 2019, alipozungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za chama hicho jijini Dar es Salaam.

Amesema, chama hicho kimekuwa kikifuatilia kwa makini mchakato wa uandikishaji tangu mwanzo, na kwamba mwitikio hafifu wa wananchi unatoa ujumbe mkubwa kwa Serikali ya Rais John Magufuli.

“Tumekuwa tukifuatilia mchakato wa uandikishaji wa wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi, kumewa na mwitikio mdogo sana,” amesema.

Amesema, chama hicho kilifanya juhudi kuhamasisha wananchi kujiandikisha, hata hivyo juhudi hizo zilikumbana na vikwazo kutoka Jeshi la Polisi.

“Chama chetu kiliendelea na njia mbadala zikiwemo kusambaza vipeperushi na kutumia Radio za kijamii katika maeneo mbalimbali za nchi, ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wajiandikishe,” amesema.

Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi, ikiwa ni pamoja na kujiepusha ushabikiwa kisiasa.

“Tunamtaka IGP (IGP Simon Sirro) aliongoze jeshi la polisi liwe la kwanza kutii sheria bila shuruti, badala ya kuimba ngonjera kwa umma,” amesema.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!