Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Matinyi aanika mafanikio sekta ya utalii miaka mitatu ya Samia, Tz kinara Afrika
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Matinyi aanika mafanikio sekta ya utalii miaka mitatu ya Samia, Tz kinara Afrika

Watalii wakiwa moja ya mbuga nchini Tanzania
Spread the love

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema katika kipindi cha uongozi wa miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, utalii ndio sekta inayoongoza kwa kuiletea nchi fedha za kigeni ambapo sasa zimefikia dola za Marekani bilioni 3.37 (zaidi ya Sh 8 trilioni). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema kimsingi sekta hiyo imemrejeshea shukurani Rais Samia kwa juhudi zake binafsi za kutoka ofisini na kwenda kushiriki katika utengenezaji wa filamu ya “Tanzania: The Royal Tour”.

Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari leo Jumapili jijini Dar es Salaam, Matinyi amesema katika kipindi cha miaka mitatu idadi ya watalii nchini imeongezeka kutoka 922,692 mwaka 2021 walioipatia nchi mapato dola za Marekani bilioni 1.31 hadi watalii 1,808,205 mwaka 2023 walioingiza dola bilioni 3.37.

Ameswma idadi ya watalii walioongezeka baada ya mlipuko wa UVIKO-19, umeifanya Tanzania sasa inashika nafasi ya pili barani Afrika baada ya Ethiopia.

Amesema mapato makubwa yameongezekna na kuifanya Tanzania kushika nafasi ya tatu baada ya Moroko na Morisi (Mauritius).

“Tanzania imeendelea kutambuliwa kimataifa na kupata tuzo mbalimbali. Tuzo hizo ni Hifadhi ya Taifa Serengeti kuwa hifadhi bora barani Afrika kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2019 hadi 2023; Tanzania kuwa nchi ya saba miongoni mwa nchi 18 duniani zilizo bora kutembelewa kiutalii kwa mwaka 2022.

“Hifadhi ya Taifa Serengeti kuorodheshwa kama eneo maridhawa la kutembelewa kwa mwaka 2023; na Hifadhi ya Taifa Serengeti kushika nafasi ya tatu ya vivutio bora vya asili duniani kwa mwaka 2023,”

Aidha, amesema Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro imeshinda tuzo mbili za Best of the Best Travelers’ Choice na Africa’s Leading Tourist Destination kwa mwaka 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!