Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi TFF kuamua hatima ya Amrouche
Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Adel Amrouche
Spread the love

HATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea na kibarua chake nchini itajulikana hivi karibuni, wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakapomwita katika kikao cha kujadili mustakbali wake.

Tarehe haijapangwa lakini taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zinasema uongozi wa mpira wa miguu utakutana na Amrouche baada ya kumalizika kwa mashindano ya Fifa Series yaliyoandaliwa na Shirikisho la Miguu la Kimataifa (FIFA) yanayofanyika nchini Azerbaijan kati ya tarehe 18 na 25 Machi.

MwanaHALISI lilipata taarifa hizo lilipohoji uongozi wa TFF kwa nini wachezaji wa Taifa Stars wameitwa na kaimu kocha mkuu, Ahemed Morocco badala la Amrouche. Pili tulitaka kujua, hadi lini kocha huyo ataendelea kulipwa mshahara bila kufanya kazi.

Akijibu maswali hayo Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau alisema, “Maswali yote muulizeni Ndimbo (Clifford Mario – afisa habari wa TFF), atawapa ufafanuzi.”

MwanaHALISI lilipomtafuta Ndimbo kwa ufafanuzi alijibu, “Suala la Amrouche, TFF itakutana na kocha baada ya kumalizika michezo ya kalenda ya FIFA inayofanyika Azerbaijan ili kujadili mustakbali wake.”

Kibarua cha Amrouche kilitatizika tangu wakati wa fainali za Mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) Januari mwaka huu nchini Ivory Coast. Mwishoni mwa Januari, MwanaHALISI lilijulishwa kwamba hatima ya kocha huyo ilikuwa inasubiri kikao cha TFF baada ya kumalizika kwa fainali za Afcon.

Taarifa za kuaminika zilizopatikana kutoka ndani ya TFF zilieleza kuwa kocha huyo hana chake ndani ya shirikisho hilo na hakuna uwezekano wa kuendelea kuitumikia nafasi yake.

“Hamna mtu anayemtaka ndani ya TFF. Safari yake ishaiva yule, haponi yule, alikuwa anatafutiwa sababu na sasa imepatikana,” alisema afisa mmoja wa shirikisho. Alikuwa anajibu swali “hivi suala la kocha limekaaje, anaweza kuwa na maisha marefu kutokana na sakata hili?”

Kuvunjika kwa ndoa hiyo kulitokana na matukio kadhaa ya kocha huyo kuelekea katika fainali hizo za Afcon na zaidi ni shutuma zake dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF).

Amrouche, wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mchezo wao dhidi ya Morocco aliwashutumu FRMF kuwa wanaishinikiza CAF kuwapangia ratiba zinazowabeba ikiwa ni pamoja na kuwapangia muda mzuri wa wao kucheza mechi.

Haraka Rais wa TFF, Wallace Karia alijitokeza na kujibu kuwa huo si msimamo wa shirikisho la soka nchini bali ni maoni binafsi ya kocha. Hata hivyo, kauli hiyo haikuokoa hasira za CAF.

Kwanza, CAF ilimpa kocha huyo adhabu ya kutokusimamia Stars katika mechi nane. Pili, TFF ilitozwa faini ya dola za Kimarekani 10,000 sawa na Sh. 25 milioni. Kutokana na TFF kuadhibiwa, nalo liliamua kumsimamisha kwa muda usiojulikana.

Kwa kuwa Stars bado ilikuwa inakabiliwa na mechi mbili dhidi ya Zambia na dhidi ya DR Congo, TFF ilimkaimisha ukocha mkuu, Ahmed Morocco aliyekuwa msaidizi wa Amrouche, na pili likamteua, kocha wa timu ya wanawake ya Simba, Juma Mgunda na kumsafirisha hadi Ivory Coast kuwa msaidizi wa Morocco. Amrouche alirejeshwa Dar es Salaam kusubiri hatima yake.

Hadi kufikia Februari hakukuwa na mabadiliko yoyote badala yake TFF ilikata rufaa kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupinga adhabu ya Amrouche kufungiwa mechi nane pamoja na faini ya dola za Kimarekani 10,000 sawa na Sh. 25milioni.

Vyanzo tofauti vilithibitisha kwamba uamuzi wa TFF kukata rufaa ulikuwa na lengo la kutaka kuendelea na kocha huyo raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria ambaye aliiwezesha Taifa Stars kufuzu kucheza fainali za Afcon.

Taifa Stars ilifuzu kwa mara ya kwanza kwenye fainali za Afcon mwaka 1980, mara ya pili 2019 na mara ya tatu 2023 safari hii chini ya Amrouche.

Msukumo wa kukata rufaa, japokuwa umechelewa, ulitokana na namna CAF ilivyoamua kumfungia kocha mkuu wa Morocco, Walid Regragui kutokana na tafrani yake dhidi ya nahodha wa DR Congo, Chancel Mbemba lakini siku moja baadaye alifutiwa adhabu hiyo.

Hata hivyo, hadi sasa TFF haijapokea majibu yoyote kutoka CAF ikiwa na maana kocha ataendelea kupokea mshahara bila kazi.

Wiki iliyopita TFF ilimpa jukumu Morocco kuteua kikosi cha Taifa Stars ambacho kiliondoka Jumatatu asubuhi kwenda Azerbaijan kushiriki mashindano yatakayoshirikisha timu nne katika kundi lao ambazo ni pamoja na wenyeji, Bulgria na Mongolia.

Stars in atarajiwa kucheza michezo miwili ikianza  na  Bulgaria tarehe 22 Machi na kumalizana na Mongolia Machi 25 na itarejea nchini tarehe 27 Ma chi, 2024. Makala hii imeandaliwa na Erasto Masalu… (endelea).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!