WANAVIJIJI wa Kata ya Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara, wameamua kuanza ujenzi wa zahanati kwa nguvu zao, ili kukwepa adha ya kufuata huduma ya afya umbali mrefu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, wanavijiji hao hulazimika kutembea umbali wa kilomita 10 kwenda kupata huduma za afya kwenye Kata jirani ya Murangi.
“Kata ya Musanja yenye vijiji vitatu haina Kituo cha afya wala zahanati hata moja katika vijiji vyake, hii ndio Kata pekee jimboni kwetu yenye hali kama hiyo. Mbunge ameendesha harambee ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mabuimerafuru,” imesema taarifa hiyo.
Kupitia harambee iliyoongozwa na Prof. Muhongo, fedha kiasi cha Sh. 1,350,000 zilikusanywa, mifuko ya saruji 59 na kondoo mbili.
Prof. Muhongo alichangia mifuko 200 ya saruji, ambapo kamati ya ujenzi iliundwa.
Katika hatua nyingine, taarifa hiyo imesema zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere, inakaribia kuanza kutoka huduma na kwamba maombi yakufungiwa umeme yamepelekwa TANESCO.
Leave a comment