November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marufuku kuingia mkataba bila kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku mamalaka yeyote ya Serikali kuingia mkataba bila kuishirikisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa mikataba inayoingiwa bila kuishirikisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali lakini mgogoro unapotokea mamlaka husika kwenda kuomba msaada kwa ofisi hiyo.

Samia ametoa agizo hilo leo Alhmisi Tarehe 29, Septemba, 2022, wakati akizungumza na Mawakili wa Serikali kwenye Mkutano wao Mkuu wa Chama ambacho kimeanzishwa rasmi na kuzinduliwa jijini Dodoma.

“Kuna mikataba watu wanajiingilia tu huko halafu  ikitokea shida huko wanakimbilia kwa AG tusaidie, mliingiaje mikataba AG hajui, na pengine aliyeingia alishastaafu hayapo na pengine hayupo duniani kwahiyo kupata chanzo inasumbua kwahiyo niombe sana na hii ni kwa Serikali nzima kwamba hakuna mkataba utakaoingiwa bila kushirikisha ofisi ya mwanasheria mkuu,” amesema Rais Samia.

https://youtu.be/fLMVAMHcx9s

Aidha Mkuu huyo wan chi amewataka mawakili wa Serikali kutekeleza majuku yao kwa weledi na uadilifu katika kushuhulikia mashaur ya uwekezaji ili kusaidia kukuza uchumi na pato la Taifa.

Amewataja mawakii hao kama jeshi la kulinda uchumi wa Taifa hasa katika kipindi hiki ambacho Seerikali imehamasisha uwekezaji ambao amesema utakuja na migogoro mbalimbali ya kiuwekezaji ambayo itahitaji utatuzi.

Amesema ili kukuza uchumi ni lazima migogoro hiyo itatuliwe kwa haki na pengine ishughulikiwe kabla ya kufikishwa mahakamani iwe imetatuliwa.

error: Content is protected !!