KIMBUNGA Ian kimetokea Florida nchini Marekani na kusababisha madhara makubwa ikiwemo mafuriko. Anaripoti Helena Mkonyi TUDARCo, kwa msaada wa vyombo vya habari vya kimataifa … (endelea).
Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba miti na magari yalionekana yakisombwa na maji na baadhi ya nyumba sehemu mbalimbali ziliathiriwa ikiwemo ni pamoja na kukosekana kwa umeme.
Ian kilitua Jumatano Kusini-Magharibi mwa Florida, Wataalamu wa hali ya hewa nchini humo wamesema kuwa Kimbunga hicho kimeleta dhoruba zenye nguvu zaidi kuwai kurekodiwa Marekani.
Wanasema “dhoruba hiyo ya kiwango cha nne, ilitua karibu na Cayo Costa, Kisiwa kilichohifadhiwa Magharibi mwa Fort Myers, kikiwa na kasi ya kilomita 241 kwa saa, kikielekea Kaskazini-Mashariki mwa Pensula ya Kaskazini-Magharibi.”
Aidha serikali ya Jimbo la Florida na Marekani awali zilitoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo yaliyolengwa na dhoruba hiyo, huku wakazi wengi wakilazimika kuondoka kwenye makazi yao kwa usalama wao.
Leave a comment