Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Marekebisho sheria za uchaguzi: Chadema, ACT-Wazalendo watinga bungeni
Habari za Siasa

Marekebisho sheria za uchaguzi: Chadema, ACT-Wazalendo watinga bungeni

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), pamoja na Chama Cha ACT-Wazalendo, vimewasilisha maoni na mapendekezo Yao kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kuhusu marekebisho ya sheria za uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wawakilishi wa vyama hivyo wamewasilisha mapendekezo hayo Jana Jumamosi, tarehe 6 Januari 2024, bungeni jijini Dodoma.

Mapendekezo ya Chadema yaliwasilishwa na katibu wake Kanda ya Kati, Emmanuel Masonga, pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Wananchi la chama hicho, Lumola Steven.

Akizungumza baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo, Steven alisema Chadema kinapendekeza marekebisho hayo yatanguliwe na marekebisho madogo ya Katiba.

“Sisi wabunge wa Chadema tulijadili miswada yote vifungu Kwa vifungu, muswada wa sheria ya tume ya uchaguzi tulichambua vifungu 28, sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani vifungu 168 na ya msajili wa vyama vya siasa 30,” amesema Lumola na kuongeza:

“Baada ya kuchambua wabunge wa Chadema tulibaini hakuna namna yoyote ya kufanya marekebisho haya bila kugusia katiba.”

Kwa upande wa ACT-Wazalendo, mapendekezo yake yaliwasilishwa na Emmanuel Mvula.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyowasilishwa ni, viongozi  wa Tume ya Uchaguzi, ikiwemo mwenyekiti na makamu wake wapitie usaili wenye ushindani, tume iwe na uhuru wa kibajeti  inayotoka  kwenye mfuko wa mfuko mkuu wa hazina na usalama wa ajira  uimarishwe.

Mengine ni, tume iwe na watumishi wake hadi ngazi ya halmashauri, wakurugenzi wa halmashauri wasisimamie uchaguzi. Kamati ya usaili ifanyiwe maboresho kwa kujumuisha vyama vya siasa na ssasi za kiraia.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi badala ya TAMISEMI,  mchakato wa uchaguzi uwe huru na wa haki ikiwemo kuondolewa kwa faini kwenye mapingamizi, kumuondoa msajili wa vyama vya siasa kwenye mapingamizi na kuweka ulazima wa fomu za matokeo kukabidhiwa kwa mawakala wa vyama.

Mengine ni, vifungu vyote vinavyojinaisha siasa viondolewe na madaraka ya Msajili wa Vyama vya Siasa yapunguzwe,  Kuimarisha usawa wa kijinsia kwa kuviwekea vyama sharti la ushirikishwaji wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi (30%) na  Mabadiliko madogo ya Katiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!