BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), leo tarehe 7 Januari 2024, limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili na darasa la nne wa 2023, huku likisema ufaulu umeongezeka. Anaripoti Regina Mkonde …(endelea).
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Ally Mohamed, amesema ufaulu wa Mitihani wa kidato cha pili umeongezeka kwa asilimia 0.13 ambapo watahiniwa 592,741 (85.31%) wamepata daraja kuanzia la kwanza hadi la nne.
Aidha, Dk. Mohammed amesema watahiniwa 28 wa mtihani wa kidato cha pili wamefutiwa matokeo kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo udanganyifu na kuandika matusi.
Kwa upande wa mtihani wa darasa la nne, Dk. Mohammed amesema ufaulu umeongezeka hadi kufikia asilimia 0.39, ambapo watahiniwa 1,287,934 (83.34%), wamefaulu kuendelea darasa la tano huku wengine 178 wakifutuwa matokeo.
Leave a comment