Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yaishutumu Urusi kuinyonya Afrika kufadhili vita Ukraine
Kimataifa

Marekani yaishutumu Urusi kuinyonya Afrika kufadhili vita Ukraine

Spread the love


MAREKANI inasema mamluki wa Urusi wananyonya maliasili katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mali na Sudan ili kufadhili vita vya Moscow nchini Ukraine. Urusi imekataa shtaka hilo ni kuita ni “hasira dhidi ya Urusi”, shirika la habari la Reuters linaripoti. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, amesema kundi la mamluki la Urusi la Wagner lilikuwa likitumia “mafanikio yaliyopatikana kwa njia mbaya” “kufadhili matukio yao ya vita katika maeneo ya Afrika, Mashariki ya Kati na Ukraine”.

“Usifanye makosa: watu kote barani Afrika wanalipa gharama kubwa kwa vitendo vya unyonyaji vya Kundi la Wagner na ukiukaji wa haki za binadamu,” aliuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ufadhili wa makundi yenye silaha kupitia usafirishaji haramu wa maliasili.

Urusi inakanusha uhusiano wowote na Wagner. Kundi hilo limekuwa likifanya kazi nchini Libya tangu 2016, ambapo liliunga mkono harakati za Jenerali Khalifa Haftar juu ya serikali rasmi ya Tripoli mnamo 2019.

Mnamo 2017, Kundi la Wagner lilialikwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kulinda migodi ya almasi. Inaripotiwa pia hufanya kazi nchini Sudan, kulinda migodi ya dhahabu. (Chanzo: BBC)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!