Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mama Mongela: Mwalimu alikuwa msikivu wa wanawake
Habari za Siasa

Mama Mongela: Mwalimu alikuwa msikivu wa wanawake

Rais wa kwanza wa Bunge la Afrika, Mama Getrude Mongela
Spread the love

RAIS wa kwanza wa Bunge la Afrika, Mama Getrude Mongela amesema Hayati Mwl. Julius Nyerere alikuwa msikivu wa wanawake na alifanya mambo mengi wa ushauri na busara zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Mama Mongela ameyasema hayo leo Jumamosi tarehe 9 Aprili, 2022 katika mdahalo wa Kitaifa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwl. Nyerere.

Amesema anamwona Mwl. Nyerere kama mtu wa ajabu kwani hadi anatoka duniani hakujua mawazo yake kuhusu heshima kwa mwanamke na kwamba anashangaa kwanini hakuyatoa hadi anatoa duniani.

“Labda angeyatoa wakati wa uhai wake sisi kazi yote tuliyofanya ya kuhamasisha dunia nzima kuhusu heshima kwa mwanamke ingekuwa haina maana tena,” amesema.

Hata hivyo amesema mawazo yake kuhusu mwanamke yalionekana baadae kwenye Kitabu alichoandika akiwa mwanafunzi wa Chuo cha Makerere kinachoitwa Uhuru wa Wanawake.

“Kitabu hiki ni wachache wamekisoma, ni mawazo ya mwalimu mwaka 1944 akiwa mwanafunzi Makerere aliandika kitabu juu ya uhuru wa wanawake akichambua jamii zetu na jamii za kiafrika akiweka msingi mikubwa ambayo aliiamini ya uhuru, haki, heshima na utu wa mwanamke,” amesema Mama Mongela.

Akinukuu kitabu hicho amesema Mwl Nyerere aliandika “Wanawake mliumbwa kwa mfano wa Mungu lakini watu wamewafanya mfikiri kuwa ninyi ni kuku na nyinyi wenyewe mnafikiri hivyo, lakini ninyi ni tai nyoosheni mbawa yenu mruke, msiridhike na chakula cha kuku kwa bidiii zenu wenyewe na kwa msaada wa rafiki zenu jitoeni kwenye hali hii ya unyonge mliyonayo sasa ili mfaidi uhuru na haki katika ulimwengu wenye Amani,” mwisho wa kunukuu.

Akitoa ushahidi wa heshima ya Mwl. Nyerere kwa wanawake, Mama Mongela alisema yeye mwenyewe alimsikia alipokuwa akizungumza na akinamama kwenye mkutano.

Amesema Mwl. Nyerere alisema katika mkutano huo, anamnukuu, “mimi mwenyewe nilikuwa najisikia uchungu nilipokuwa naona mama yangu anafanya kazi, mama yangu likuwa analima akiniachia mdogo wangu Joseph kumbembeleza, nikiona mama amelima mno amechoka inabidi nimfinye alie ili nimrudishie mtoto amshike naye aweze kupumzika,” mwisho wa kumnukuu.

Julius Nyerere, Hayati Baba wa Taifa

“Thamani aliyokuwa akioona kwa mwanamke ilikuwa ya kupita kiasi” amesema Mama Mongela.

Amesema amekuwa akitafuta wanawake maarufu wa Tanzania na wengi wakiwa wale waliofanya mapinduzi tunayoyaona sasa “walitoa mawazo yaliyoijenga Tanzania tunayoiona.”

“Kwanza alipokwenda UNO alirudi na azimio kwamba Tanzania itapata uhuru baada ya miaka 12 akapeleka kwenye kamati kuu ambako na wanawake walikuwepo.

“Alikuwepo mwanamke mmoja Tatu Mzee, Mwl. alipowasilisha watu wakapiga makofi lakini yule mama akasimama akasema “Julius tafadhali unasemaje tungoje miaka 12 ndiyo tuwe huru mimi nakataa, kama ni hivyo sisi wanawake tuwameze wanaume halafu tutafute uhuru tukishapata tutawatapika tuwape viti.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!