Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mama, bintiye wahukumiwa kwa kuuza viongo vya miili ya marehemu
Kimataifa

Mama, bintiye wahukumiwa kwa kuuza viongo vya miili ya marehemu

Spread the love

MMILIKI wa zamani wa Chumba cha kuhifadhu maiti na mama yake wamehukumiwa kifungo cha jela huko Colorado baada ya kupasua mamia ya miili na kuuza sehemu za mwili. Yameripoti Mashirika ya Habari ya Kimataifa…(endelea).

Waendesha mashtaka walisema Megan Hess, 46, na Shirly Koch, 69, walikata maiti 560 na kuuza viungo vya miili bila idhini kati ya 2010 na 2018.

Wanawake wote wawili walikiri makosa ya ulaghai mapema mwaka huu.

Hess atafungwa jela 20, huku Koch akihukumiwa miaka 15 jela.

Kulingana na waendesha mashtaka huko Colorado, wawili hao mama na binti walivuna sehemu za miili, na wakati mwingine miili mizima katika na kuviuza.

Hess – ambaye aliendesha biashara ya Jumba la Mazishi la Sunset Mesa katika mji wa Montrose – alitoza familia hadi $1,000 (£834) kwa uchomaji maiti ambao haukufanyika na badala yake kuikabidhi miili hiyo kama michango bila malipo , waendesha mashtaka walisema.

“Wanawake hawa wawili waliwadhulumu wahasiriwa ambao waliwageukia wakati wa huzuni,” Leonard Carollo, ajenti maalum wa FBI anayesimamia Denver, alisema katika taarifa.

“Lakini badala ya kutoa mwongozo, wanawake hawa wenye pupa walisaliti imani ya mamia ya wahasiriwa na kukata viungo vya wapendwa wao’

Kesi hiyo ilichochewa na uchunguzi wa Reuters, ambao ulisababisha FBI kuvamia nyumba hiyo mwaka wa 2018. Ni kinyume cha sheria nchini Marekani kuuza viungo, lakini uuzaji wa viungo vya mwili kwa sasa haudhibitiwi na sheria ya shirikisho ya Marekani.

Taarifa za waathiriwa waliojawa hisia zilitawala kikao cha hukumu cha Jumanne.

“Wakati Megan alipoiba moyo wa mama yangu, alivunja moyo wangu,” alisema Nancy Overhoff, kulingana na Denver Post. Erin Smith alisema: “Tumekuja leo kusikia pingu zikikazwa.”

Akiielezea kama “kesi ya kuhuzunisha zaidi ambayo nimewahi kukumbana nayo kwenye benchi”, Jaji Christine Arguello aliamuru wanawake hao wawili wafungwe gerezani mara moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

Kimataifa

Urusi, Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita

Spread the loveJUMLA ya wafungwa 179 wa kivita wa Urusi na Ukraine...

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

error: Content is protected !!