WIZARA ya mambo ya nje nchini Ufaransa, imethibitisha kupokea barua kutoka serikali ya Burkina Faso, inayomtaka balozi wake nchini humo Luc Hallade kuondoka. Inaripoti Mitandao ya Kimaifa (endelea).
Kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza na mwandishi wa Gazeti la Le Monde nchini Ufaransa, kilichosababisha uongozi wa kijeshi kumfukuza Balozi huyo, ni taarifa aliyotoa kuhusu tahadhari za kiusalama kwa raia wa nchi yake katika mji wa Koudougou kilomita 100 kutoka jiji kuu la Ouagadogou.
Taarifa hiyo iliwataka raia hao kuondoka kwenye mji huo kurudi jiji kuu au mji wa Bobo Dioulasso kwa sababu za kiusalama, maelekezo ambayo hayakupokelewa vema na serikali ya Burkina Faso.
Paris imekosoa hatua hiyo ikisema ni kinyume cha taratibu kati ya serikali na kuongeza kuwa licha ya kupokea barua ya Balozi wake kutimuliwa, bado yupo jijini Ouagadougou.
Hatua hii ya Burkina Faso inakuja pia baada ya kumfukuza Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Barbara Manzi kwa madai kuwa kauli yake kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini humo, ilikuwa ni kwa nia mbaya kuonesha kuwa uongozi wa kijeshi haufanyi vya kutosha kuimarisha usalama wa nchi hiyo.
Leave a comment