Katibu wa NEC – Itikadi na Uenezi (CCM) Paul Makonda amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe ni mnufaika mkubwa wa maridhiano ya kisiasa kati ya CCM na Chadema kwani ndio yamefanya kuwa huru baada ya kuachiwa bila masharti katika kesi mbalimbali huku kesi zote za kisiasa zikifutwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Amesema Mbowe anafahamu katika mapendekezo 84 yaliyotolewa, mapendekezo 63 yote yamechukuliwa na yapo kwenye miswada ambayo hatua za kisheria zinaendelea ili kuwa sheria kamili.
“Pia chama chake na vingine vikaruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara bila kubughudhiwa tena kwa mlinzi mkali chini ya Jeshi la Polisi kuhakikisha dhamira ya Rais Samia inatimia si tu kwa vyama vya siasa bali kwa Watanzania wote.
Aidha, ameongeza kuwa kila alichosema Mbowe, Rais Samia aliridhia na wakati mwingine alikubali kukinzana na wana CCM wenzake ili kujenga mustakabali mpana wa Taifa moja lisilobaguana na vyama.
“Lakini matokeo yake jana Mbowe katangaza tena kuacha mchakato huu wenye dhamira njema na kukimbia mtaani kuhamasisha maandamano” amesema Makonda.
Leave a comment