Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo yalia na machinga Arusha
Habari za Siasa

ACT Wazalendo yalia na machinga Arusha

Spread the love

CHAMA Cha ACT-Wazalendo kimeitaka Serikali kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara ndogondogo maarufu ‘machinga’ yatakayowawezesha kufanyabiashara zao na si kuwakimbiza na kuwamwaga bidhaa zao. Anaripoti Faki  Sosi, Arusha (endelea).

Akizungumza leo tarehe 14 Januari 2023 katika uzinduzi Mkutano Mkuu wa chama hicho wa mkoa wa Arusha ulioambatana na uchaguzi wa viongozi wa mkoa huo,  Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Dorothy Semu amesema kuwa kitendo cha wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga cha kunyanyaswa na askari wa jiji hakivumiliki.

“Hiki ni kilio cha nchi mzima sisi ACT -Wazalendo  tunataka kujenga taifa litakalowaheshimu wafanya baishara wanawekewa mazingira mazuri biashara zao zitastawi, watafanya biashara kwa amani “

Amesema kuwa kisingizio cha kuwa wafanyabiashara wanachafua miji hakikubaliki.

“Tunasimama na wafanyabiashara tunaitaka Serikali  ya Arusha kuhakikisha wanaweka mazingira bora kwa ajili ya wafanyabiashara.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

error: Content is protected !!