Sunday , 5 May 2024
Habari za SiasaTangulizi

Makonda kizimbani leo

Paul Makonda
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania leo Jumatano tarehe 2 Machi 2022, itasikiliza maombi ya kufungua kesi ya jinai dhidi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda. Anaripoti Mwandishi WetuDar es Salaam … (endelea).

Maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo na mwandishi mkongwe nchini humo, Saed Kubenea.

Kesi hiyo iliahirishwa tarehe 8 Februari 2022 na Hakimu, Aron Lyamuya anayeisikiliza ambapo alitoa uamuzi wa kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa Makonda.

Lengo ni ili kumwezesha Makonda kupata taarifa za kesi iliyofunguliwa na Kubenea baada ya jitihada za kumpata ili kumpa wito wa kuhudhuria mahakani kushindikana.

Katika kesi hiyo, Kubenea anawakilishwa jopo la mawakili wakiongozwa na Nyaronyo Mwita Kicheere na Hekima Mwasipu.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Makonda anadaiwa kuwa siku ya tarehe 17 Machi 2017, akiwa na watu waliobeba silaha za moto, alivamia Clouds TV na kumuagiza mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu kurusha video inayomwonesha mwanamke aliyejulikana kwa jina la Grace Athuman.

Katika video hiyo, ambayo haijulikani nani ameiandaa, mwanamke huyo alidaiwa kuonekana akifanya tendo la ndoa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Kwa mujibu wa ushahidi wa video za CCTV, Makonda anaonekana kuvamia kituo cha Clouds saa nne usiku, akiwa anaendesha mwenyewe gari namba T553BFM.

Vilevile, Camera za CCTV pamoja na kitabu cha kumbukumbu za walinzi, vinamuonesha Makonda aliingia Clouds akiwa na askari wanne waliokuwa na sare tofauti za majeshi ya ulinzi na usalama, kati yao watatu wakiwa na silaha za moto.

Askari hao waliingia hadi chumba cha utangazaji, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za utangazaji, huku Makonda akitumia vitisho dhidi ya wafanyakazi wa Clouds kwa kutumia silaha za moto.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo ya Kubenea, kitendo cha Makonda cha kuvamia televisheni ya Clouds, tena akiwa ameongozana na askari waliobeba silaha za moto, ni kinyume cha sheria ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2010.

Saed Kubenea

Maombi ya kutaka kumshitaki Makonda yamewasilishwa mahakamani, chini ya kifungu cha 99 (1) cha Sheria ya mwenendo wa mashauri ya Jinai, Sura ya 20.

Kubenea ambaye amewahi kuwa mbunge wa Ubungo (Chadema), katika Bunge lililopita anasema, hatua ya Makonda kuvamia Clouds, ni matumizi mabaya ya madaraka, chini ya kifungu cha 96 ya Kanuni ya adhabu (Penal Code), Sura ya 20 na kuingilia moja kwa moja, mawasiliano ya Kieletroniki.

Mbali na Makonda, wengine walioitwa mahakamani siku hiyo, ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Wawili hawa wanadaiwa wameshindwa kuchukua za kumfungulia mashitaka ya jinai mtuhumiwa huyo.

Kubenea amefungua maombi ya kufungua kesi ya jinai dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Makonda mwenyewe.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Aron Lyamuya ambaye ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 2 Machi 2022.

Ametoa uamuzi huo baada ya mawakili wa Kubenea, Nyaronyo Kicheere na Hekima Mwasipu kuiomba mahakama kutoa samasi ya kumtangaza kwani jitihada za kumpata Makonda ili kupatiwa wito wa kufika mahakamani kugonga mwamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!