September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makamu wa Rais Marekani aambukizwa Corona

Spread the love

MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris imebainika ameambukizwa virusi vya Corona licha ya kupatiwa dozi zote mbili za chanjo ya Covid – 19. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani, jana tarehe 26 Aprili, imesema Makamu huyo wa Rais alikamilisha dozi zote mbili za Covid- 19za chanjo aina ya Moderna Covid-19.

Chanjo hizo alizipata kwa mara ya kwanza mwishoni mwa Oktoba, 2021 na dozi ya pili alipata Aprili 1 mwaka huu.

Makamu huyo wa Rais amepata maambukizi ya Covid-19 ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Serikali ya Marekani ilipopunguza vikwazo dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa sheria za Afya ya Jamii wageni wote na maafisa hawaruhusiwi tena kuvaa barakoa au kujitenga katika shughuli mbalimbali katika Ikulu ya Marekani White House.

Taarifa za maambukizi ya Covid-19 jijini Washington Marekani zimepungua kwa asilimia kubwa tangu zilipotikisa zaidi mapema mwezi Januari ambapo Serikali ilikabiliana na kesi nyingi za maambukizi hayo.

Licha ya kwamba Ikulu ya Marekani imekuwa ikiendelea kufanya shughuli zenye kuhitaji watu wengi uvaaji wa barakoa umekuwa ni hiari na maafisa wengi kutoka White House wamesahau kabisa suala zima la kuvaa barakoa mbele ya hadhara.

Kumekuwa na sheria ya lazima kupimwa kwa wale wanaokutana moja kwa moja na Rais Joe Biden na wanalazimika pia kukaa naye mbali katika vikao na mikutano mbalimbali.

Katibu wa Habari wa Ikulu ya Marekani White House, Jen Psaki amedai kuwa Ikulu hiyo haina mpango wa kurudi enzi za kuweka vikwazo juu ya tahadhari za kujikinga na maambukizi ya Uviko-19.

“Tunaendelea kutekeleza sera ya watu kurudi kuwajibika makazini na tunahisi kuwa tuna sababu za kufanya hivyo,” alisema Psaki.

error: Content is protected !!