Spread the love

WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ameishauri Serikali ya Tanzania kufuata nyayo za Serikali ya Zanzibar, kukuza uchumi kwa kutumia rasilimali za bahari, kupitia sera ya uchumi wa buluu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Jaji Warioba ametoa ushauri huo leo Jumanne, akihutubia katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika jijini Dodoma.

Jaji huyo mstaafu, ameishauriu Serikali ya Tanzania, iweke mpango wa kitaifa juu ya matumizi ya rasilimali za bahari, ikiwemo samaki kwa ajili ya chakula. Mafuta na gesi asilia.

“Uchumi wa buluu sio la Zanzibar peke yake, ni la nchi nzima. Tunayo bahari, ni rasilimali tuna sehemu ya bahari mashariki mwa Pemba, Unguja na Mafia maili 200, ni ukanda wa uchumi wa nchi. Kuna rasilimali madini inawezekana kuna mafuta na gesi,” amesema Jaji Warioba.

Jaji Warioba amesema “lakini kubwa kuna samaki, dunia watu wanaongezeka vyanzo vya chakula vinapungua bahati sehemu moja wapo chanzo kikubwa cha chakula ni bahari tuliyo nayo. Walka tusije tukaiacha Zanzibar ikawa na uchumi wa buluu, lazima uwepo mpango wa kitaifa.”

Aidha, Jaji Warioba amempongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, kwa kuipa kipaumbele sera ya uchumi wa buluu.

“Mimi ningefikiri ambapo Serikali zote mbili lazima tushirikiane ili wananchi wapate kipato, kuna maeneo mengi tuchukue mfano wa uchumi wa buluu. Hii nampongeza Rais wa Zanzibar kwa kuweka mkazo,” amesema Jaji Warioba.

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *