WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mbio za NMB Marathon 2022 yanayotarajiwa kufanyika Oktoba mosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Mashindano hayo yanayoratibiwa na Benki ya NMB yamesogezwa mbele ili kukidhi maombi ya washiriki wengi ambapo hapo awali yalipangwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana katika uzinduzi wa ‘kits’ vifaa vya mbio hizo, Meneja Rasilimali Watu wa benki hiyo, Emmanuel Akonaay alisema mashindano hayo yanalenga kuchangia matibabu ya fistula kwa wanawake kupitia Hospitali ya CCBRT.
Alisema katika mbio hizo ambazo zitashirikisha wadau wa aina mbalimbali, jumla ya Sh milioni 600 zimepangwa kukusanywa ili kusaidia matibabu ya akina mama wenye matatizo hayo ya fistula.
“Kwa siku 10 hizi zilizobaki tunaomba Watanzania na wadau mbalimbali na kampuni, kujisajili kushiriki mbio hizi ili kuchangia matibabu hayo,” alisema na kuongeza kuwa kauli mbio ya mbio hizo ni ‘mwendo wa upendo’.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya NMB Marathon, Mercy Nyange alisema hadi kufikia jana Septemba 20, 2022 jumla ya washiriki 3000 wamejisajili katika mbio hizo.
“Tunawaomba Watanzania na wadau mbalimbali kusogea pale Juliana Pub Mbezi Beach, Mtana Bar au Mlimani City kwa siku hizi 10 zikizobaki ili wajisajili na kuwa kwenye orodha rasmi ya wale watakaokimbia kwenye NMB Marathon 2022,” alisema.
Leave a comment