Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Msigwa: Mchakato marekebisho ya sheria unakwenda vizuri
Habari Mchanganyiko

Msigwa: Mchakato marekebisho ya sheria unakwenda vizuri

Spread the love

MSEMAJI Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema mchakato wa marekebisho ya sheria zinazosimamia sekta ya habari nchini, unaendelea na kwamba umefikia hatua nzuri. Anaripoti Regina Mkonde… (endelea).

Msigwa ametoa kauli hiyo hivi karibuni, alipoulizwa hatua iliyofikiwa kuhusu marekebisho ya sheria za habari, tangu Rais Samia Suluhu Hassan, alipoagiza sheria hizo zifanyiwe marekebisho ili kuondoa vifungu vinavyolalamikiwa na wadau kuwa ni kandamizi.

“Subirini mtapewa taarifa, lakini unakwenda vizuri. Mtajulishwa,” alisema Msigwa.

Akihutubia wadau wa vyombo vya habari kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, tarehe 3 Mei 2022, jijini Arusha, Rais Samia alimuagiza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, aendeshe majadiliano ya wadau kwa lengo la kupata mapendekezo ya namna ya kuzifanyia marekebisho ya sheria hizo, kwa kuzingatia maslahi ya pande zote, Serikali na wanahabari.

Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mwishoni mwa Agosti, 2022, Nape alisema mchakato huo unaendelea.

Mchakato huo umezidi kupamba moto Novemba 2021, baada ya wadau mbalimbali, wakiongozwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kwa kushirikiana na Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kuwasilisha mapendekezo yao serikalini kuhusu marekebisho hayo.

Mapendekezo hayo yanahusu marekebisho ya sheria za habari, ikiwemo Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015, Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya 2016, Sheria ya Takwimu ya 2015, iliyofanyiwa marekebisho 2019 na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kuondolewa mamlaka ya kusimamisha au kufuta leseni za magazeti, haki na wajibu wa vyombo vya habari, uanzishwaji wa Bodi ya Wanahabari, Mfuko wa Habari na Baraza Huru la Habari Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!