Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa aipongeza Tunduma kwa ukusanyaji mapato
Habari za Siasa

Majaliwa aipongeza Tunduma kwa ukusanyaji mapato

Spread the love

 

WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kuridhishwa na kasi ya ukusanyaji mapato uliopo katika halmashauri ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe huku akimsisitiza mkurugenzi wa mji huo, Philimon Magesa kuendeleza kasi hiyo bila kujali figisu zilizopo. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Majaliwa ametoa pongeza baada ya Mkurugenzi huyo kudaiwa kuminya mianya ya wizi wa fedha za halmashauri katika ukusanyaji mapato ambapo baadhi ya watendaji walizoea kula fedha mbichi wakiendesha ushawishi kwa baadhi ya madiwani ili kuendesha hujuma ili aonekane hafahi.

Waziri mkuu ambaye yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Songwe amewaeleza wananchi kupitia mkutano wake kuwa mkurugenzi huyo ameaminiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na ndiyo maana yupo Tunduma na kasi ya ukusanyaji mapato imeonekana.

Alisema wakati anaingia kufanya kazi katika halmashauri hiyo alikuta makusanyo ya fedha za mapato ya ndani ni Sh bilioni tano lakini kwa muda wa mwaka mmoja wa uongozi wake mapato yameongezeka na kwamba katika mwaka huu wa fedha amefanikiwa kukusanya Sh bilioni nane kabla hata ya  mwaka wa fedha haujaisha.

‘’Madiwani mlindeni mkurugenzi wenu, ametumia akili kubwa kuifanya halmashauri hii kupaa kimapato, sitegemei kuibuka migogoro, wakuu wa Idara ongereni sana, kwa kazi nzuri na ushirikiano mlio nao kwa madiwani.

“Kitendo cha kukusanya fedha kubwa kabla ya muda mnapaswa kupongezwa,nataka wakurugenzi wa halmashauri zingine ikiwemo Lindi jimboni kwangu waje kujifunza Tunduma’’alisema Waziri mkuu Majaliwa.

Mbunge wa jimbo la Tunduma ,David Silinde

Naye Mbunge wa jimbo hilo,David Silinde alisema anafahamu uwezo wa mkurugenzi huyo toka alipokuwa halmashauri ya wilaya ya Nzega ambapo alifanikiwa kukusanya mapato maradufu.

Amesema ujio wake kwenye halmashauri ya mji Tunduma, kwake haukuwa na shaka na sasa wameona matunda katika vyanzo hivyo hivyo ameweza kuvuka lengo kabla hata mwaka wa fedha haujamalizika.

Aidha, Silinde ambaye ni Naibu waziri katika ofisi ya Rais (TAMISEMI ) anayeshughulikia elimu,amesema kutokana na makusanyo hayo wameweza kujenga miradi mbalimbali mikubwa zikiwemo shule za ghorofa na miradi ya afya kwa mapato ya ndani.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji Tunduma, Philimon Magesa ameishukuru Serikali kwa kumuamini na kwa jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewapatia vinu na mitambo ya kuzalisha gesi kwa ajili ya matumizi ya hewa ya Oxjeni itakayotumika kusaidia wagonjwa wenye uhitaji.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!