Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Tax aongoza aongoza ujumbe wa Tanzania mkutano wa mawaziri AU
Habari za Siasa

Dk. Tax aongoza aongoza ujumbe wa Tanzania mkutano wa mawaziri AU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax
Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023.

Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 18-19 Februari 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pamoja na mambo mengine, mkutano wa Mawaziri utajadili masuala ya kimkakati yanayohusu Bara la Afrika ikiwemo utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika-AfCFTA, uhakika wa chakula, hali ya ulinzi na usalama, mabadiliko ya tabianchi, pamoja na masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.

Akichangia katika mkutano huo, Dk. Tax alisisitiza umuhimu wa Kamisheni na Taasisi za Umoja wa Afrika kusimamia vyema rasilimali za Umoja wa Afrika kwa kuchukua hatua za kuondoa mapungufu yaliyobainika kwenye taarifa ya ukaguzi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.

Waziri Tax pia alieleza hatua ambazo Serikali ya Tanzania inachukua katika kutekeleza Mikataba ya Uenyeji ya Taasisi za Umoja wa Afrika zilizopo Tanzania ambazo ni Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Umoja wa Posta Afrika na Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri dhidi ya Rushwa.

Awali akiwasilisha hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Moussa Faki Mahamat alisisitiza umuhimu wa Umoja wa Afrika kuendelea kutoa kipaumbele kwenye masuala yanayowagusa wananchi wa Afrika .

Pia kutatua changamoto mbalimbali za mabadiliko za kijamii, kiuchumi na kiusalama. Alisisitiza umuhimu wa Afrika kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za vyakula ndani ya bara la Afrika pamoja na kutumia fursa za mkataba wa AfCFTA katika kukuza Mtangamano wa Kiuchumi.

Faki aliongeza kuwa Umoja wa Afrika umeendelea kusimamia masuala ya amani na usalama katika bara la Afrika katika nchi za Ethiopia, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Libya ambapo jitihada zilizofanyika zimelenga zaidi kupata suluhisho la amani kwa mataifa hayo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Demeke Mekonnen amesema Ethiopia ameshukuru Umoja wa Afrika kwa mchango na ushirikiano wake ambao umewezesha kupatikana amani na utulivu nchini Ethiopia na kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka miwili. “Ethiopia inaamini kuwa kupitia Umoja wa Afrika amani, ulinzi na usalama vitailetea Afrika maendeleo zaidi,” alisema Mekonnen.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!