Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Watanzania watakiwa kutojitumbukiza kwenye mikopo bila malengo
Habari Mchanganyiko

Watanzania watakiwa kutojitumbukiza kwenye mikopo bila malengo

Spread the love

WATANZANIA  wameshauriwa kutopenda kujitumbukiza kwenye masuala ya mikopo kama hawajajipanga kwa kujua wanachotakiwa kukifanya. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 14 Februari 2023 na  Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC), Dk. Beng’i Issa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma Juu ya utekelezaji wa Baraza hilo.

Mbali na kuwataka watanzania kutojitumbukiza katika mikopo ambayo hawajajiandaa nayo pia amewataka watanzania kuwa na nidhamu ya fedha sambamba na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba yakita benki.

Akizungumzia ufanisi wa baraza hilo, Beng’i ameeleza kuwa kazi kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kihuchumi.

Katika kutilia mkazo juu ya kuwawezesha wananchi ameeleza kuwa kwa sasa kuna mifuko mbalimbali ya kuwawezesha akina mama na vijana huku akieleza kuwa akina mama wamekuwa wakipewa kipaumbele zaidi kwa kuwa ni waaminifu katika kurejesha.

“Nataka kuwaeleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana baraza kwa kushirikiana na serikali kwa ujumla wake wametoa kiasi cha Sh. 5.6 trilioni kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wapatao milioni nane jambo ambalo ni hatua kubwa katika kuwawezesha watanzania kujiinua kiuchumi” ameeleza Beng’i. 

Sambamba na kutoa pesa hizo kwa ajili ya kuwawezesha watanzania milioni nane Beng’i amesema kuwa bado watanzania wengi wanakabiliwa na elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Kutokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha amesema kuwa serikali kwa kushirikiana taasisi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa watanzania ili kuhakikisha watanzania wanajikwamua katika maisha na kuishi maisha ambayo yatakuwa bora kila mmoja jambo ambalo litawafanya watanzania kuwa na amani na furaha,” amesema Beng’i.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!