Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Magonjwa 10 yaliyochangia vifo vingi 2018
Afya

Magonjwa 10 yaliyochangia vifo vingi 2018

Spread the love

SERIKALI imetaja magonjwa kumi yaliyochangia vifo kwa mwaka 2018 huku ugonjwa wa shinikizo la damu ukijitokeza katika magonjwa hayo na kuchangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pia imesema magonjwa hayo kumi yamesababisha vifo 20,087 mwaka 2018 ikilingishwa na vifo 19,693 kwa mwaka 2017.

Hayo yaliyobainishwa jijini hapa jana na Waziri wa Afya Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari hali ya huduma za afya nchini katika kipindi cha mwaka 2018.

Ummy aliyataja magonjwa hayo kumi kuwa ni Homa ya mapafu ambayo ilisababisha vifo kwa asilimia 12.9, kukosa pumzi kwa watoto asilimia 6.3, ugonjwa moto asilimia 6.2, kifo cha mtoto tumboni(Ngozi imechubuka) asilimia 3.8 na Maralia asilimia 3.4.

Magonjwa mengine ni Ukimwi asilimia 3, kifo cha mtoto tumboni ngozi haijachubuka asilimia 2.7, magonjwa mengine asilimia 2.7, maambukizi katika damu kwa watoto asilimia 2.5 na shinikizo la damu asilimia 1.9.

Kuhusu huduma ya tiba nchini alisema, kwa mwaka 2018, jumla ya mahudhurio ya wagonjwa wliofika katika vituo vya kutolea huduma za afya walikuwa milioni 42.4 ikilinganishwa na milioni 54.4 kwa mwaka 2017.

Waziri alisema, kati ya hao wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 41.052 na wagonjwa wa kulazwa walikuwa 1,359,264 na kwamba takwimu hizo zinajumuisha wagonjwa wa hudhurio la kwanza na mahudhurio ya marudio.

Aliwataja wagonjwa waliohudhuria katika hospitali za halmashauri, vituo vya afya na zahanati katika ngazi ya msingi kwa wagonjwa wa nje ilikuwa 36,376,967.

Akizungumzia magonjwa ya mlipuko alisema, Tanzania imeendelea kuwa salama licha ya tishio la kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa Wizara kuchukua tahadhari ya kulinda mipaka yake.

Ummy alifafanua kuwa kutokana na tahadhari hiyo Tanzania haikuwa na magonjwa yeyote aliyegundulika kuwa na ugonjwa huo katika kipindi cha mwaka 2017 na mwaka 2018.

Kwa upande wake mganga mkuu wa Serikali, Muhamad Kambi, alisema, siku za usoni wagonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza yataweka mzigo katika sekta ya afya hivyo Wizara imeweka mkakati kwa kuanzisha mpango wa Taifa wa kudhibiti wagonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!