November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM akabidhiwa mfumo wa kusimamia mawasiliano, atoa maagizo

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 18 Januari 2019 amekabidhiwa rasmi Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) unaosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ambao ulianza kufanya kazi tangu mwezi Oktoba mwaka 2013. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika ofisi za TCRA zilizoko jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameagiza TCRA na vyombo vya dola kuuboresha na kuulinda mfumo huo.

Aidha, Rais Magufuli ameiagiza TCRA kuuboresha mfumo huo ili uweze kufuatilia mienendo ya mawasiliano ya mitandao ya kijamii, ikiwemo Skype, WhatsApp pamoja na mitandao ya kuratibu usafirishaji abiria, Uber na Taxfy.

“…Biashara ya kimtandao kuhusu masuala ya usafiri, Ubber na Taxfy , upigaji simu wa Whtasap na Skype, sina uhakika kama mfumo huu utakuwa na uwezo wa kufuatilia. TCRA iimarishe mfumo huo ili kuweza kufuatilia mitandao hiyo,” amesema Rais Magufuli.

Hali kadhalika, Rais Magufuli ameitaka TCRA kuhakikisha kila mtanzania anasajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole, ili kukomesha vitendo vya uhalifu wa mtandaoni.

Katika hata nyingine, ameagiza mamlaka za ukusanyaji kodi kufuatilia kampuni zinazotengeneza vifaa vya kielektroniki ili zitoe mchango wa fedha kwa serikali kwa ajili ya kushughulikia athari zinazotokana na vifaa hivyo baada ya kumalizika matumizi yake.

“Nchi yetu ina vifaa vingi vinavyotumia mtandao, na nifahamu kwa muijubu wa sheria watengenezaji wana wajibu wa kutoa mchango ili vitakapomalizika kutumiaka viharibiwe. Muanze kufuatilia kampuni zinazotengeneza vifaa hivyo ili viweze kutimiza majukumu yao kwa mujibu a sheria za kimataifa,” ameagiza Rais Magufuli.

Vile vile, Rais Magufuli ameagiza Wizara ya fedha kuhakikisha taasisi za umma zisizounganishgwa kwenye Mfumo wa Malipo ya Serikali Kimtandao (GePG).

“Wizara ya fedha kuhakikisha taasisi zote zinaunganishwa na mfumo wa serikali wa malipo, taasisi 339 kati ya 667 zimeunganishwa zingine bado, sasa waziri (Dk. Isdore Mpango) uko hapa nitashangaa sana hizi taasisi ambazo ni mali ya serikali ziendele kukaa bila kuunganishwa mfumo huu, nitashangaa mawaziri na makatibu wakuu wa taasisi hao kama wataendelea kufanya hivyo itakuwa na maana wanataka kuendelea na biashara za gizani kama alivyosema spika,” amesema Rais Magufuli.

Akielezea manufaa ya mfumo huo, Rais Magufuli amesema TTMS utasaidia kuongeza mapato kupitia kodi zinazotokana na mawasiliano ya simu, kufuatilia miamala ya kifedha inayofanyika kwa njia ya mtandao, kuhakiki mapato yatokanayo na huduma ya mawasiliano ya simu, kubaini mawasiliano ya simu za kimataifa.

Amesema tangu mfumo uanze kutumika hapa nchini, umeleta faida nyingi , ikiwemo kufahamu takwimu sahihi za watumiaji wa simu pamoja na kuipatia serikali zaidi ya Sh. 93 bilioni ambapo 82 bilioni zimepelekwa hazina na 11 bilioni zimepelekwa katika Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)

Licha ya mafanikio hayo, Rais Magufuli ametahadharisha juu ya athari za mitandao, na kuiitaka TCRA kuwa mbogo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya kw akutumia sheria zilizopo ili kuhakikisha vitendo hivyo vinakoma.

error: Content is protected !!