Saturday , 11 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Madiwani Songwe wachachamaa mradi wa milioni 600 kukwama
Habari Mchanganyiko

Madiwani Songwe wachachamaa mradi wa milioni 600 kukwama

Spread the love

MADIWANI katika halmashauri ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe, wamemjia juu meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) wa halmashauri ya mji huo, wakitaka kujua sababu ya kukwama kwa mradi wa maji uliotolewa fedha zaidi ya Sh. 600 milioni. Anaripoti Ibrahim Yassi, Songwe …(endelea).

Serikali kuu ilitoa fedha hizo miaka miwili iliyopita lakini umedaiwa kusuasua kwa zaidi ya mwaka mmoja huku vifaa vya ujenzi vikidaiwa kuibiwa hali iliyodaiwa kurudisha nyuma jitihada za serikali za kumtua mama ndoo kichwani.

Akizungumza kuhusu sakata hilo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichokaliwa jana tarehe 2 Mei 2023 Diwani wa kata ya Chipaka, Hamis Shombe amesema kwa muda mrefu kata ya Majengo, Msongwa na mtaa wa Nyerere hakuna maji.

Amesema uhaba huo wa maji safi uliilazimu serikali kutoa fedha za kujenga mradi huo eneo la Nyerere na ulitakiwa ukamilike Septemba mwaka 2022 lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea huku baadhi ya saamani ikiwemo nondo zikiibiwa.

Naye Diwani wa kata ya Majengo, Frank Mponzi alisema mradi huo ni muhimu kwa wananchi lakini anashangaa kuona umemaliza mwaka mmoja bila kazi kufanyika.

Alisema hadi sasa mifuko ya saruji 24 na nondo 25 ziliibiwa na wao kama viongozi wa kata walimkamata mtuhumiwa wa wizi na kumpeleka polisi huku akiomba ufafanuzi kwa kwenyekiti wa halmashauri akisema jitihada za serikali za kumtua mama ndoo kichwani zinaweza kukwama.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji huo, Ayoub Mlimba alimuagiza meneja wa RUWASA Anthon Modest kutoa ufafanuzi.

Akitoa ufafanuzi wa kukwama kwa mradi huo, Kaimu meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) wilayani Momba, Anthon Modest alikiri mradi huo kukwama na kuongeza kuwa walibaini mkandarasi aliyepewa zabuni hiyo hana uwezo.

 

Alisema kutokana na kasoro hizo, waliamua kumuondoa mkandarasi huyo na kumpa mkandarasi mwingine ambaye tayari ameanza kazi na ifikapo tarehe 30 Juni 2023, mradi utakamilika na kuhusu wizi wa vifaa na uchakavu wa bomba alisema wameanza kufanyia kazi.

Mahitaji ya maji halmashauri ya mji Tunduma wenye wakazi 159,493, ni lita za ujazo milioni 11,164,510 kwa siku.

Hadi kufikia Septemba 2022 uzalishaji wa maji ulifikia lita za ujazo 5,219,550 sawa na asilimia 45.75 ya mahitaji jitihada bado zinahitajika kumaliza tatizo la maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

Spread the loveMBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta...

error: Content is protected !!