Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Abdul Kambaya ang’atuka Chadema,”mimi sio wa kwanza kuondoka”
Habari Mchanganyiko

Abdul Kambaya ang’atuka Chadema,”mimi sio wa kwanza kuondoka”

Spread the love

MWANASIASA maarufu nchini Abdul Kambaya ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa zimepita siku 52 tangu alipojiunga na chama hicho akitokea Chama cha Wananchi -CUF. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Kambaya ametangaza uamuzi huo leo tarehe 3 Mei 2023, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Defrance iliyopo Sinza wilayani Ubungo.

Pamoja na mambo mengine amesema “Ninaondoka Chadema na sitojiunga na chama chochote. Kwa sasa mimi  ni mwanasiasa huru.”

Amesema kuondoka kwake CHADEMA sio jambo jipya kwa Mtanzania yeyote kujiunga katika chama na kisha kuondoka.

“Kama Lowassa na Sumaye walijiunga na CHADEMA na wakatoka, siwezi sema kuna changamoto hasi zilizonifanya kuchukua hatua hii ya kutangaza kujitoa Chadema. Sijitoi Chadema kwenda chama kingine cha siasa,” amesema Kambaya.

Amesema itakapofikia mwaka 2025 atafanya uamuzi wa kurejea kwenye siasa na kuangalia chama atakachojiunga nacho.

Kambaya ameongeza kuwa tangu walipojiunga CHADEMA tarehe 11 Machi mwaka huu akiwa na wanachama wenzie zaidi ya 400, walipokewa vizuri na wala hawakupata changamoto hasi zozote.

Amesema mazingira na mafanikio ya kisiasa yaliyopo CHADEMA ndio yaliyoleta changamoto kwake kuendelea kuwa mwanachama wa chama hicho.

Itakumbukwa kuwa tarehe 11 Machi 2023 Kambaya na wafuasi wake 402 walitangaza kujiunga CHADEMA na kupokewa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alijinasibu kukiimarisha  chama katika ukanda wa kusini ambao waliuachia CUF ambacho nacho kimesuasua.

Hata hivyo, baadae zaidi ya wanachama 200 wa CUF walijiunga CHADEMA na kumfuata Kambaya aliyekuwa Mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!