Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali: Mchakato wa kuandaa muswada wa sheria ya habari umefikia 80%
Habari Mchanganyiko

Serikali: Mchakato wa kuandaa muswada wa sheria ya habari umefikia 80%

Spread the love

SERIKALI za Tanzania Bara na Zanzibar zimesema mchakato wa kupatikana kwa Sheria ya Habari yenye kukidhi mahitaji ya wadau upo katika hatua za mwisho. Anaripoti Selemani Msuya, Zanzibar …(endelea).

Hayo yamesemwa na leo tarehe 3 Mei 2023 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Tabia Maulid Mwita na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Celestine Kakele wakati wa kizungumza na wadau wa habari Kisiwani Zanzibar katika kongamano la Maadhimisho la mika 30 ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD).

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Tanzania.

Waziri Mwita amesema kwa upande wa Zanzibar mchakato wa sheria hiyo umefikia asilimia 80, hivyo ni matarajio yao asilimia iliyobakia itakamilika muda mchache ujao.

Amesema Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amedhamiria kuweka mazingira rafiki kwa tasnia ya habari, kutokana na mchango wake kwenye kuchochea shughuli za maendeleo nchini.

“Mchakato wa kuandaa muswada wa sheria ya habari umefikia asilimia 80, hivyo asilimia 20 ilibaki tunaendelea kuimalizia, naamini kama kungekuwa hakuna mvutano kila kitu kingekuwa sawa kwa sasa, lakini niwahakikishieni kuwa Serikali ya SMZ chini ya Rais Mwinyi haitawaangusha, nyie ni wadau muhimu sana,” amesema.

Aidha, Waziri Mwita amewataka waandishi wa habari kutumia siku ya WPFD kujadili namna ambavyo watashiriki kutokemeza changamoto ya uwepo wa habari zisizo za kweli.

“Naomba kuwasihi mshirikiane kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu tulionao, mshirikiane katika kufanikisha utoaji wa habari sahihi na za kweli kwa umma,” alisema Tabia.

Kwa upande wake Naibu Katibu Kakele amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa vyombo vya habari katika kutimiza mipango ya maendeleo nchini na kwamba wizara imedhamiria kukamilisha mchakato wa mapitio ya sheria itakayoboresha mazingira ya vyombo vya habari haraka iwezekanavyo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Celestine Kakele akiandika michango ya wadau wa habari wanaoshiriki Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD), yanayofanyika kitaifa Kisiwani Zanzibar

Amesema sheria hiyo itazingatia maslahi ya waandishi wa habari na nchi, huku akiwataka waandishi kuzingatia wajibu na mipaka ya kazi zao.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Mussa Juma maboresho Sheria ya Habari yazingatie uwepo wa maslahi ya waandishi wa habari.

Juma amesema hakutakuwa na maana iwapo waandishi wanaadhimisha WPFD huku kundi kubwa la kada hiyo likitumikishwa kinyume cha sheria za ajira.

“Maadhimisho ya WPFD ni muhimu kwetu lakini, hayatakuwa na maana kama asilimia 80 ya waandishi hawana mikataba ya ajira, lazima tubadilike kuhakikisha tunashirikiana kukomboa kundi hili muhimu katika kuelezea mafanikio na changamoto za serikali,” amesema.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe amesema kuwa wanatambua na kuthamini kuimarika kwa uhuru wa vyombo vya habari kwa siku za karibuni, ila bado hatujafikia mafanikio makubwa.

Shebe amesema hayo wakati akitoa hotuba yake mbele ya wadau wanaoshiriki WPFD ambapo aliweka bayana kuwa sekta ya habari ni kichocheo cha maendeleo hivyo ipewe kipaumbele.

Amesema maadhimisho hayo ambayo yana kaulimbiu ‘Kuunda Mustakabali wa Haki, Uhuru wa Kujieleza kama Kichocheo cha Haki nyingine Zote za Kibinadamu’ ni vema ikawatafakarisha wanahabari namna wanaweza kuendelea kuhamasisha kuwepo kwa uhuru wa kujieleza.

Shebe amesema waandishi wanapaswa kujadiliana mambo ambayo yatawavusha kutoka walipo na kuelekea kwenye fursa nzuri zaidi ambapo uhuru wa uhariri, kutafuta habari, kuhoji na kujieleza  vinakuwa ni suala ambalo   kila Mtanzania anapaswa kujivunia.

Aidha, amewakumbusha waandishi kuwa pamoja na kudai uhuru wa vyombo vya habari, wafahamu kwamba hakuna uhuru usio na mipaka, hivyo wanapaswa kuzingatia misingi ya taaluma na maadili pamoja na kujali faragha za watu wakati wakitimiza majukumu yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

error: Content is protected !!