Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Mabondia wa Tanzania kunolewa Cuba
Michezo

Mabondia wa Tanzania kunolewa Cuba

Spread the love

 

TANZANIA kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Serikali ya Cuba kupitia Taasisi ya INDER ya nchini humo zimekubaliana kushirikiana katika eneo la kuendeleza mchezo wa ngumi, ambapo mabondia kutoka nchini watapata fursa ya kuweka kambi Cuba.

Pia walimu wa ngumi na Mabondia kutoka Cuba watapata fursa ya kuja Tanzania kufundisha na kubadilishana ujuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Makubaliano hayo yamefikiwa juzi tarehe 2 Agosti 2023 wakati Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamis Mwinjuma alipofanya mazungumzo na Raul Fornes Valenciano ambaye ni Makamu wa Rais wa kwanza wa Taasisi hiyo ya Kitaifa ya Michezo, Elimu na Burudani ambacho ni chombo kinachohusika na ukuzaji wa michezo, elimu ya viungo na burudani nchini Cuba.

Taasisi hiyo tayari ina mashirikiano na baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Algeria ambapo hubadilishana uzoefu kwenye eneo la mchezo wa ngumi.

Naibu Waziri Mwinjuma yupo nchini Cuba kwa ajili ya kuhudhuria maonesho ya kimataifa ya michezo ya Havana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!