Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Nitafuta sheria hizi nikiingia Ikulu
Habari za Siasa

Lissu: Nitafuta sheria hizi nikiingia Ikulu

Spread the love

TUNDU Lissu, mbombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameahidi kufuta sheria zote kandamizi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Ametoa ahadi hiyo jana Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020, akiwa kwenye kampeni za kusaka urais zilizofanyika katika viwanja vya Relini, jijini Arusha.

“Tanzania ya Tundu Lissu baada ya tarehe 28 Oktoba, tutafanya marekebisheo makubwa katika mfumo wa kisheria kuhusu kesi za jinai na nitafanya haraka kabisa,” alisema Lissu.

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara alisema, endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, atarekebisha mfumo wa sheria kuhusu kesi za jinai, ili kuondoa sheria zinazonyima watuhumuwa dhamana, hasa wa utakatisha fedha na uhujumu uchumi.

“Kitu kikubwa ambacho kinasababisha mateso haya ya makesi ya uongo chanzo kikubwa ni kwamba, kuna masheria ya ukandamizaji ambayo yametengeza makosa yasiyokuwa na dhamana, ukipigwa utakatishaji fedha unaozea gerezani hakuna dhamana,” alisema Lissu.

“Tanzania ya Tundu Lissu itafuta sheria zote zinazonyima watu dhamana, Katiba yetu inasema, mahali kila mtu anahesabika kuwa hana hatia hadi hapo hatia yake itathibitishwa mahakamani, maana yake kama Katiba inasema huna hatia, hutakaa gerezani sababu umetuhumiwa tu.”

Lissu aliahidi kuifuta machozi nchi ya Tanzania pamoja na kurudisha umoja wa wananchi hasa wa jiji la Arusha.

“Arusha ya ujana wangu ilikuwa Arusha ya amani, ilikuwa Arusha ya upendo na watu kusaidiana, Arusha ya leo ya watu ambao wanateswa kwa miaka mitano, wamenyang’anywa pesa zao.”

“Arusha ya leo ni ya machozi damu na  vilio kwa sababu ya ukandamizaji wa miaka mitano, baada ya tarehe 28 Oktoba nitafuta machozi ya Arusha, nitafuta machozi ya Tanzania,” aliahidi Lissu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!