Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Leseni uchimbaji madini ya ‘rare earth’ yatambulishwa rasmi, ajira 3000 zaja
Biashara

Leseni uchimbaji madini ya ‘rare earth’ yatambulishwa rasmi, ajira 3000 zaja

Spread the love

WANANCHI wa Wilaya ya Songwe wametambulishwa uwepo wa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini ya Rare Earth Elements yanayotumika katika teknolojia ya kisasa.

Madini hayo yametajwa kuwa yataisaidia dunia kupunguza changamoto ya athari za hewa ya ukaa kwa kutumia teknolojia safi itokanayo na madini hayo na kuepuka athari za mazingira kwa watu na mimea. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa katika hafla ya kutambulisha rasmi kwa wananchi leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini hayo katika Kijiji cha Ngwala wilayani Songwe.

Amesema madini ya Rare Earth Elements ni miongoni mwa madini muhimu na ya kimkakati yanayohitajika duniani hususan katika matumizi ya maendeleo ya teknolojia ikiwemo utengenezaji wa betri za magari ya umeme, vifaa vya simu, mota na teknolojia za kisasa.

Aidha, Dk. Kiruswa amesema uwekezaji katika mradi wa Ngualla unatarajiwa kugharimu zaidi ya Dola za Marekani 486 milioni na utazalisha ajira rasmi 800.

Pia utazalisha ajira zisizo rasmi 3,000 katika kipindi cha ujenzi wa mradi ambapo baada ya kukamilika kwa mradi utazalisha ajira rasmi 250 na ajira zisizo rasmi 1,000.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda amemuomba Dk. Kiruswa kushughulikia kero na changamoto zilizopo katika sekta hiyo mkoani humo ikiwemo miundombinu ya barabara pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme.

“Mradi wa Ngualla ulisainiwa tarehe 17, Aprili, 2023 Ikulu jijini Dodoma na tunaamini mradi ukianza uzalishaji asilimia kubwa ya vijana wetu watapata ajira na mapato ya mkoa wa Songwe yataongezeka,” amesema Itunda.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philipo Mulugo alisema Kampuni ya Peak Rare Earth Elements ina mahusiano mazuri na jamii inayozunguka eneo la mgodi.

Alisema mpaka sasa kampuni hiyo haijaanza uzalishaji lakini tayari imejenga shule, kituo cha afya, barabara na imepanga kujenga kituo cha Polisi na nyumba ya mkuu wa kituo katika Kijiji cha Ngwala.

Naye, Meneja Mkazi wa Kampuni ya Peak Rare Earth Elements, Ismail Diwani alisema Kampuni ya Peak Resources ilianza utafiti wa Phosphate  katika eneo hilo mwaka 2008.

Alisema mwaka 2010 iligundua uwepo wa tani 890,000 za madini ya Rare Earth Elements yenye kiwango bora duniani na kuachana na utafiti wa awali ili kuanza tafiti za madini ya Rare Earth Elements ambao ulikamilika mwaka 2017.

Diwani alisema mwaka 2018 Kampuni hiyo iliamua kubadilisha jina kuwa Peak Rare Earth Elements ambapo sasa kampuni hiyo inamilikiwa kwa ubia kupitia Kampuni ya Mamba kati ya Serikali kwa asilimia 16 na Peak Rare Earth Elements kwa asilimia 84.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!