Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mdhibiti ubora ashangazwa na miundombinu St Anne Marie
Elimu

Mdhibiti ubora ashangazwa na miundombinu St Anne Marie

Spread the love

SHULE ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam imepongezwa kwa kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya shule na kufanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Elikana Manyilizu ambaye ni Mdhibiti Ubora wa Shule wa Manispaa ya Ubungo, wakati wa mahafali ya 20 ya shule ya msingi yaliyofanyika shuleni hapo.

Pia aliwapongeza Maafisa wote wa Elimu wa wilaya ya Ubungo (Afisa Elimu kata- Msigani, Afisa Elimu Wilaya ya Ubungo na wasaidizi wao kwa kusimamia vizuri sana Elimu ndani ya Wilaya hiyo ya Ubungo.

Alisema usimamizi mzuri wa viongozi hawa unachangia sana shule hiyo ya St. Anne Marie Academy kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.

“Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatambua mchango mkubwa wa shule ya St. Anne Marie Academy pamoja na shule nyingine za binafsi, tutaendelea kuweka mazingira rafiki ili kupata shule nyingi ziweze kuwekeza kwenye elimu na kutoa huduma zilizotukuka kama za St. Anne Marie Academy,” alisema.

Elikana Manyilizu ambaye ni Mdhibiti Ubora wa Shule wa Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam kwenye mahafali yao yaliyofanyika shuleni hapo siku ya Jumamosi

Alisema ana imani kuwa mafanikio hayo makubwa ya shule yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wafanyakazi wa shule hiyo, kujituma, kufanya kazi kwa bidii na uwekezaji mkubwa uliofanywa na uongozi wa shule, Naomba msirudi nyuma endeleeni kufanya kazi zenu kwa bidii ili shule hii iendelee kupaa siku hadi siku.

Aliwapongeza wanafunzi wanaohitimu  kwa kufanikiwa kuifikia siku hiyo na kwamba walikuwa na nidhamu nzuri, mlikuwa mnasoma kwa bidii, mlifanya vizuri sana katika mitihani mbalimbali. Kwa mwenendo huu ni matumaini yangu kuwa mtafanya vizuri sana katika mitihani ya Taifa Mnayotarajia kufanya hivi karibuni.

“Napenda kupongeza sana uongozi wa shule kwa usimamizi mzuri wa shule. Sote ni mashahidi kwamba shule hii inafanya vizuri sana kitaaluma kwa kupata matokeo mazuri sana katika mitihani ya Taifa. Nimesikia hapa kwenye taarifa kwamba matokeo ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita ni mazuri sana,” alisema.

Alisema matokeo haya makubwa  yanaonesha ni kwa jinsi gani shule hii imejipanga kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanaohitimu hapa wanapata matokeo mazuri sana na kwamba hilo ni jambo kubwa sana na serikali inatoa pongezi kubwa.

Wakati huo huo, shule ya Msingi na Sekondari, St. Anne Marie Academy kwa mara nyingine imesisitiza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja atakayerudishwa nyumbani kwa kushindwa kulipa ada baada ya kufiwa na mzazi.

Wanafunzi wa shule ya msingi St Anne Marie Academy wakiwaburudisha wageni kwa nyimbo za bongo fleva walipofika kwenye mahafali ya 20 ya shule hiyo siku ya Jumamosi

Msimamo huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza, kwenye mahafali yha 20 ya shule ya msingi  yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

“Kwa mwaka 2021 pekee  wazazi 40 walifariki lakini watoto wao wote wanaendelea na shule hakuna hata mmoja ambaye amefukuzwa. Tumeona tufanye hivi kwasababu baada ya mzazi au mlezi kufariki watoto wanahaingaika sana,” alisema Dk. Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijinini (CCM).

“Mpango huu ulianza mwaka 2019  na mwaka 2020 wakati wa korona wazazi 42 walikufa ilikuwa ni kilio kikubwa sana kwetu na kwa watoto tukaona tubuni mpango mwanafunzi akishaingia hapa St Anne Marie akafiwa na mzazi wake au mlipa ada ataendelea kusoma hapa hatafukuzwa,” alisema

Wanafunzi wa shule ya msingi St Anne Marie Academy wakikata keki kwenye mahafali ya 20 ya shule hiyo yaliyofanyika siku ya Jumamosi shuleni hapo

Dk. Rweikiza alisema jambo lingine wanalojivunia ni kuwalea wanafunzi hao kwenye maadili ya hali ya juu na kwamba hali hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa katika kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya kiwilaya, mkoa  na yale ya kitaifa.

Alisema kuna viongozi wa dini zote ambao wamekuwa wakitoa mafundisho ya dini na wanafunzi wote wanalazimika kuhudhiria ibada za imani zao kila zinapokuwa kwenye shule hiyo.

“Hapa tunafundisha kama hatuna akili nzuri kwasababu kazi yetu ni kufaulisha tu kila mwaka tunahakikisha wanafunzi wanafaulu kwa viwango vya hali ya juu hatutaki wazazi walipe ada wasifurajie matokeo mazuri,” alisema

Pia Dk. Rweikiza alisema wataendelea kuibua vipaji vya wanafunzi ili wawe watu maarufu kwa kufanyakazi za sanaa kama muziki wa kuimba, mitindo na fasheni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!