Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jeshi la polisi lapiga marufuku maandamano UVCCM
Habari za SiasaTangulizi

Jeshi la polisi lapiga marufuku maandamano UVCCM

Spread the love

JESHI la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) katika wilaya zote nchini  kwa kufafanua kuwa yataleta vurugu na hofu kwa Watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Maandamano hayo yameitishwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida kwa lengo la kuiunga mkono Serikali kuhusu uwekezaji wa kampuni ya DP World katika bandari ya Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime imesema pamoja na utaratibu huo wa kisheria, kuitisha maandamano nchi nzima ni sawa na kutaka kuleta vurugu na hofu kwa watanzania bila sababu yeyote ile.

Amesema yapo majukwaa ya kuwasilisha jambo lolote lililo katika utaratibu wa kisheria bila kuhamasisha maandamano ya aina hiyo.

“Leo Julai 16, 2023 kupitia Vyombo vya habari mbalimbali ikiwepo mitandao ya kijamii

ameonekana Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) akitoa taarifa ya

kuhamasisha maandamano katika Wilaya zote na wataanza na Dar es Salaam Julai

18,2023 ili kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari.

“Sheria ipo wazi kwa mtu au kikundi cha watu kinapotaka kuitisha maandamano taratibu zipi

zinatakiwa kufuatwa,” amesema.

Amesema kwa msingi huo, Jeshi la Polisi Tanzania linapiga marufuku maandamano hayo yasifanyike na hii ni pamoja na watu wengine pia wenye nia kama hizo na badala yake wawasilishe hoja zao kupitia mikutano na vyombo vya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!