Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Hati 500,000 za kimila kupatikana katika wilaya 6
Habari Mchanganyiko

Hati 500,000 za kimila kupatikana katika wilaya 6

Spread the love

WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia mradi wa Uboreshaji Usalama wa Miliki za Ardhi (LTIP) inakusudia kupanga, kupima na kusajili hati za hakimilki za kimila 500,000 katika halmshauri sita nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Katika zoezi hilo, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma inatarajiwa kunufaika na mradi huo kwa kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi katika vijiji 60.

Baadhi ya wadau wa mradi wa LTIP wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya halmashauli ya Chamwino Jijini Dodoma (hayupo pichani) Chamwino Jijini Dodoma


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gift Msuya alipokuwa akifungua mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilayani hapa.

Msuya amesema kwamba wizara ya ardhi, kupitia mradi huo iliichagua Chamwino kuwa miongoni mwa wilaya sita ambazo ni Mufindi, Songwe, Mbinga, Maswa na Longido.

“Mradi huu umeanza kutekelezwa na halmashauri yetu na ndio maana leo tumekutana hapa ili kujadili rasimu na hatimaye  tuipitisha rasimu hii na kuwa mpango wa matumizi ya ardhi ya Wilaya ya Chamwino,” ameeleza.

Aidha, amesema kwamba  halmashauri ya wilaya ya Chamwino inakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo yameibuliwa katika rasimu ya mpango huo ikiwemo ukosefu wa usalama wa milki za ardhi na ukuaji wa kasi wa miji vijiji usiodhibitiwa.

Ameeleza kuwa  matatizo mengine ni ukuaji wa mji wa Chamwino kuelekea katika ardhi za vijiji, upotevu wa bionuai na uharibifu wa mazingira, uzalishaji mdogo wa mazao ya kilimo na ufugaji na uhaba wa malisho ya mifugo.

Amesema  tatizo lingine ni mfumo dhaifu wa ukusanyaji na utupaji taka ngumu na taka za kawaida, ubovu wa barabara katika baadhi ya maeneo, uhaba wa maji kwa baadhi maeneo, upungufu wa  baadhi ya huduma za jamii kama vile shule za msingi, sekondari, zahanati na vituo vya afya kwa baadhi ya maeneo.

“Nawaomba mchukue mradi huu kama fursa kwenu na kutoa ushirikiano thabiti ili kufanikisha utekelezaji wake na kutatua changamoto hizi kwani maeneo mengi yalitamani kupata fursa kama hii lakini kutokana na uchache wa rasilimali hawakufanikiwa kufikiwa na mradi” amesisitiza  Msuya

Meneja Urasimishaji ardhi ya vijiji kupitia mradi huo, Joseph Osana amesema mradi umelenga kuboresha usalama wa milki za ardhi kwa kupanga, kupima na kusajili milki za ardhi zipatazo milioni 2.5

Ambazo zinajumuisha hati milki 1,000,000 na leseni za makazi 1,000,000 katika maeneo ya mijini na hati za hakimilki za kimila 500,000 vijijini.

Mmoja wa wanufaika wa mradai huo Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’ambaku, Juma Muyeya ameishukuru serikali kwa mradi huo kwakuwa umesaidia kumaliza mgogoro baina ya kijiji chake na kijiji jirani cha Chiboli uliodumu kwa zaidi ya mika 40.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!