August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Korea Kaskazini yazidi kuichokonoa Japan

Moja ya kombora la Korea Kaskazini baada ya kurushwa

Spread the love

KOREA Kaskazini imeendelea kuichokonoa Japan kwa kurusha kombora lingine la masafa marefu ambalo linasadikika limedondokea katika bahari ya Japan, anaandika Catherine Kayombo.

Kombora hilo lililorushwa kutoka Bangyon Kaskazini mwa mkoa wa Pyongan lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40, siku ya Jumanne.

Tokyo imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan, lakini hawakueleza madhara yaliyosababishwa na kombora hilo.

Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake katika miezi ya hivi karibuni, hili likiwa kombora la 11 mwaka huu, kufuatiwa jaribio lake la mwisho mwezi Mei ilirusha makombora yake katika nyakati tofauti yote yakielekezewa bahari ya Japan.

Kombora hilo limerushwa ikiwa ni siku moja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuzungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe na Rais wa China, Xi Jinping kuhusu Korea Kaskazini.

Viongozi hao walithibitisha jitihada zao za kuhakikisha kuwa hakuna utumizi wa nyuklia katika nchi ya Korea Kaskazini.

error: Content is protected !!